Wamelipwa mara mbili
Mayonga pia alizungumzia utekelezwaji wa makubaliano ya malipo kutoka kwa tajiri huyo, akisema tangu Pili alipoondoka Novemba 25 mwaka jana, wamepokea malipo mara mbili, yaani miezi miwili.
“Na yenyewe tulipiga sana kelele ndipo akalipa mara ya kwanza Sh100,000 mwezi wa pili akalipa Sh200,000 na akaleta na kanzu ya mzee, mfuko mmoja wa ngano. Fedha hiyo tulitumia kununua ng’ombe mmoja na kondoo,” anasema.
“Lakini tangu wakati huo, kila tukimpigia simu anatuambia hali ni ngumu kwa kuwa mvua inanyesha hivyo hawaendi mtaani kuomba.”