Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

jiheshimu. kwa watu wote . kujitolea.

Ipo siri ya kuwepo katika hali hizo, ndipo utakapokuwa huru kwa kila jambo. kuwa ni mwenye kujiheshimu na kuwaheshimu wengine ni kitu kizuri. Lakini ujue hakuna mtu anaweza kwenda peke yake.
 
Tunahitaji kukua na kuonekana kwa kila mtu. Wengine wanatengeneza nguo tunazovaa, wengine wanalima mashamba kwa ajili ya kupata chakula, wengine wanajenga nyumba ili tuweze kuishi ndani , wengine wanatengeneza barabara kwa ajili ya kufanya usafiri uwe rahisi, wengine wanatufanya tufurahi kwa ajili ya kuimba kwao. mwingine amekuambia wewe kusoma ukurasa huu.
 
Kila Mtu Anamuhitaji Mwenzake.

Wakati mwingine ugumu wa wazi ni kwamba , vyovyote unavyoona kwa mwingine HIO NI BORA iko ndani mwako. ni aina ya upendo. Ni mtu kumjua mtu mwingine. Unafikiri mtu fulani ni Smart, funny, ana mafanikio, mwema , mpole, anaonekana vizuri, au ana nguvu?
 
Unazo hizo sifa ndani yako. na kama huwezi kuona hivyo vitu kwa mtu, basi unahitaji kujibadilisha ili kuwa na uzoefu wa hizo sifa. kama mtu anakukasirikia au hana utulivu kwako. ni kitu kisichostahili , inabidi kujitahidi ndani yako kuona kitu gani kinaonekana kwako
 
Nimeamua kuvuta pumuzi ili kuona ndani yangu kama yupo mtu anayeniudhi, na kama niliwahi kufahamu kabla , au nimefanya kitu kibaya . Imenishangaza kutambua kuwa nina tabia kama hilo . nilichofanya ni kuelewa . na kuanza kubadilika .
 
Nimejua kuwa kila unachoona kwa mtu , ndicho unachokuwa nacho . sasa nkila ninapomwona huyu mtu naonyesha upendo na furaha. Ni vizuri kufanyia kazi maisha na kujali watu ili kuwa na afya nzuri .
 
Wakati mwingine sio jinsi tunavyojiona, ila ni mahali ambapo tunahitaji kukua. Kama upo kwenye nafasi ya mtu ambaye hakuheshimu , labda kwa sababu fulani, inaweza kuwa ni swali ulilojiuliza. kuwa unajiheshimu kwa kiwango gani?
 
Kama ulikuwa na mtu ambae alikusaliti, na ilikuwa ni uchaguzi wako, ungejiona kama muathirika, ungesema ; masikini, masikini mimi. au ungetazama kwa mtazamo mwingine mgumu kwamba namna gani umejisaliti. na kuona kwamba ulitegemea kitu tofauti na hakipo kwa huyo mtu cha kuonyesha vitendo.
 
Kwa hio umejisaliti mwenyewe kwa kupanga vitu ambavyo havikustahili kwenye mahusiano yenu. kwa hio hujasalitiwa ila umejisaliti mwenyewe. kwa hio badilika , fanya bidii ya kuona mazuri kwa mwingine ili yaonekane kwako.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Fayaaa
[emoji91] [emoji91]
[emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91]
Fayaaaa

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nlienda kukutafuta celebrity skukuona leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…