Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matatizo hujenga uwezo kwa baadhi ya watu, sisemi kuwa mtu akumbatie matatizo. hio ni mbaya kama kumshughulikia Adui.Lakini nasema kutana nayo kama rafiki,kwa kuona mengi na ukawa na muda mzuri wa kuyaongelea hayo ni vema.
 
Mara nyingi tumekuwa tukiamini kwamba kama huna kila kitu kwa sasa, ni tatizo. Wakati mwingine unaweza kujihisi kama umepigwa kichwani na kila baya na kuona kama umetupwa nje ya ulimwengu. ukweli ni kwamba-na inachukua nguvu kupata haya mawazo-Kila kitu katika maisha kipo hapa kutuokoa ili tuwe watu bora. ingawa sio kuwa wakamilifu, ila kwa ubora ule tutakaokuwa nao.
 
Tunaweza kushindwa kukabiliana nayo, ingawa tunaweza kuepuka mahangaiko,Lakini mara zote tuko kwenye nafasi ya kutumia tulivyo navyo na tusivyokuwa navyo ili kujiendeleza na kuonyesha ubora uliopo ndani mwetu.
 
Niliwahi kukutana na” jaribu ” na liliniogopesha sana .Nikaja kuelewa kuwa kila kitu kinachotokea kwetu kina sababu.lakini jaribu hili lilikuwa na changamoto na lilichukua muda mwingi.niliumia kihisia.
 
Ilitokea katika njia yangu, mama mmoja ambaye alikuwa akienda kwenye clinic ya maumivu kila mara. ingawa maumivu yangu hayakuwa ya kimwili, alikuwa na neno sahihi la kunitia moyo.lakini alinipa zaidi. tulipokuwa tukiongea kuhusu hali halisi, nilimtazama na kumuuliza swali, ” kwa hio ilitokeaje haya yote? ” alinitazama kama vile nimemuuliza 2+2 na alijibu kwa urahisi tu ” ili uweze kukua!”
 
Kukua sio kitu ambacho ni comfortable kwa kila mtu. ndio maana tunasikia kuhusu ” kukua kwa maumivu”ukiwa umekua bila maumivu, unaweza kwenda kwa ulaini sana. lakini haina maana kwamba umekaa na kukubali kila kinachotokea bila ya kufanya mabadiliko wakati nyakati ngumu zinapopiga.
 
Unahitaji kushughulika;kufanya uamuzi ulio sahihi kwako, kubadilisha mtazamo wako jinsi unavyoona vitu, na kuendelea wakati unapofika.
 
Mtazamo ni jibu.

Mtazamo ni Uchaguzi

UNAPATA KUCHAGUA JINSI UNAVYOTAZAMA KILA SIKU, MAHUSIANO, HALI YOYOTE, JAMBO, .UNAPATA KUCHAGUA MATARAJIO YAKO KILA PUNDE.

MFANO.
 
Kundi la vyura walikuwa wanacheza siku moja wakati wa jua, wakati wanaruka ruka chura moja akangukia shimoni. akaanza kuita msaada” help, help!” alilia huku akijaribu kuruka ili atoke juu. rafiki zake wakazunguka na kumsihi aruke juu zaidi, lakini alikuwa chini sana . walichanganyikiwa watawezaje kumtoa mwenzao.
 
Akaja mfalme wao aliposikia sauti za kelele na kufikiria wazo. akawaambia waanze kutupia mawe ndani alipo chura ili atumie kupanda . wakati mawe yanaendelea kutupiwa ndani na kumpiga huyo chura, alianza kulia , hakuweza kufikiria kwa nini maisha yamekuwa hivyo kwake.
 
Akachukia .akaanza kuyakwepa mawe kila yanapoingia na kupanda juu yake. wakati mwingine yanampiga na kuanguka lakini anarukia juu na kutambua kuwa anakaribia kufika juu ya shimo. haikuchukua muda mawe yakafika juu na yeye akaweza kuruka nje
 
Kitu alichofikiria kuwa kinamuumiza ndicho kilichomtoa chura juu ya lile shimo. alimshukuru mfalme kwa kuleta hilo wazo na kwa wema wake.
 
Changamoto za maisha ni ya kiisometriki kwa ajili ya nafsi.husukuma nje nguvu ya ndani. kwa kila magumu, huangalia cheche na kuleta yale yote ya uwezo wako. kama hutapata cheche, furahia maajabu zaidi ya ufahamu wako.

MAZURI AU MABAYA NANI AJUAYE?
 
Mzee mmoja na kijana wake waliishi kijijini na walikuwa na shamba dogo na farasi mmoja tu, ambae ndio alikuwa akivuta jembe la kulimia. siku moja farasi alikimbia na kupotea.
 
Majirani walimuonea huruma sana , na kusema ” jinsi gani imekuwa hivyo. mbona bahati mbaya hivyo.!

mzee wa watu alijibu , nani ajuaye kama ni ” bahati mbaya au nzuri?”.
 
Baada ya wiki moja Farasi alirudi akifuatana na farasi wengine watano kutoka mlimani.

Majirani wakasema, ni bahati ya kushangaza sana.

Lakini mzee akajibu, nani ajuaye kama ni BAHATI MBAYA? AU NI BAHATI NZURI?
 
Siku iliofuata kijana alijaribu kumfunga moja wa farasi wao, alianguka na kuvunjika mguu.
 
BAHATI MBAYA ? AU BAHATI NZURI?

Wanajeshi walikwenda kijijini hapo kwa ajili ya kukusanya vijana kwenda vitani, mtoto wa yule mzee alikuwa hawezi kutumiwa tena , alionekana hana maana kwao, kwa hio akapona kwenda vitani

Nzuri? au Mbaya?
 
Back
Top Bottom