Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matumizi yao hayazidi kipato
Tathimini kubwa ya ukomavu wa mwanaume ni kwa kutazama matumizi yake ya pesa.

Mwanaume mchanga hutumia pesa nyingi kuliko zile anazozipata; kwake vitu kama kununua nguo, simu ya bei, kuhonga wanawake, na pombe ni vitu vya msingi zaidi kuliko kuweka akiba au kuwekeza.

Lakini hali hii ni kinyume kwa wanaume waliokomaa kwani wao huweka akiba, hutumia kidogo kuliko wanachopata tena kwa mambo ya msingi na hufikiri kuhusu kuwekeza.
 
Sio wanaume pekee wanaopenda kuangalia video za ngono, utafiti uliofanywa nchini Uingereza umebaini kuwa mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu wamekiri kuangalia video hizo walau mara moja kwa wiki.

Na wengi wamedai kuwa huziangalia kwa kutumia simu za mkononi.

Mpiga picha wa Uingereza, Amanda de Cadenet aliungana na Marie Claire kufanya utafiti kwa wanawake wa kisasa na uhusiano wao na video hizo na kubaini kuwa wengi wao ni watazamaji wazuri na tena huangalia wakiwa peke yao, kwa raha zao, kuliko wakiwa wenzao wao.
 
Matumizi yao hayazidi kipato
Tathimini kubwa ya ukomavu wa mwanaume ni kwa kutazama matumizi yake ya pesa.

Mwanaume mchanga hutumia pesa nyingi kuliko zile anazozipata; kwake vitu kama kununua nguo, simu ya bei, kuhonga wanawake, na pombe ni vitu vya msingi zaidi kuliko kuweka akiba au kuwekeza.

Lakini hali hii ni kinyume kwa wanaume waliokomaa kwani wao huweka akiba, hutumia kidogo kuliko wanachopata tena kwa mambo ya msingi na hufikiri kuhusu kuwekeza.
 
Hawayumbishwi na maneno ya wanawake
Umezaliwa peke yako, umekua peke yako, unakuja kuyumbishwa na mtu ukiwa na miaka 18+? Hii si sawa hata kidogo.

Wanaume waliokomaa wanatambua na kuthamini nafasi ya mwanamke kwenye maisha yao, lakini hawaruhusu maneno mabaya ya wanawake yawatishe.

Maneno kama vile “wewe siyo mwanaume mzuri”, “huna hadhi yangu”, “hufai kuwa mume”, “huna hela”, n.k. ni baadhi ya maneno mabaya ya wanawake ambayo mwanaume aliyekomaa haathiriwi nayo.
 
Hawabebi chuki na hasira
Chuki na hasira huathiri afya ya mwili, roho na hata utendaji wako wa kazi. Kubeba chuki hakukusaidii bali kunaendelea kukutesa huku kukimwacha aliyekukwaza akiendelea na maisha yake.

Wanaume waliokomaa huwa na moyo wa kusema acha yapite au yaishe; kisha huendelea na maisha na shughuli zao za kila siku.
 
Hawajihisi wadhaifu juu ya mwonekano wao
Mwanaume hasifiwi sura bali anasifiwa kwa mafanikio au malengo aliyoyatimiza. Wanaume waliokomaa hawajali kuwa mimi nina sura mbaya au mimi sina mvuto kama wa fulani n.k.

Nikukumbushe pia kuwa masuala kama vile kunyoa kiduku, kuvaa milegezo au kuiga kila mtindo wa mavazi ni maswala ya kivulana tena ya wanaume wachanga ambao hawajakomaa.

Wanaume waliokomaa hutafuta mafanikio halisi, tena ya kudumu na siyo vitu vya nje kama vile sura au mvuto kwa wanawake.
 
Hawakai mbali na familia zao
Ukimwona mwanaume ambaye anakimbia familia yake, huyo bado ni mchanga sana. Fahari ya mwanaume yoyote aliyekomaa ni kuona yuko karibu na anaihudumia familia yake kila mara.

Kama baba yako au mkeo anakutunzia kila kitu cha familia yako sasa kwanini usiitwe mwanaume suruali? Mwanaume aliyekomaa hujali wajibu wake na kuhakikisha anakaa katika nafasi yake kama baba wa familia.
 
Back
Top Bottom