Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Imagine umetoka job halafu unamkuta waifu kakaa anatabasamu tu halafu hakusemeshi. Mi nageuza aisee hata ndani siingii [emoji16][emoji16][emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Utageuza kimya kimya pasipo kumsemesha???

Kuna mwanaume aliwahi muacha mpenzi wake kwasababu ya hofu*
Mwanaume alikuwa mchepukaji sana na kila akichepuka mpenziwe anagundua, kamfuma kama mara 3 na wapenzi tofauti anamsamehe...Mwanaume kaogopa kuendelea nae kwa kudhania kuwa anatunzwa tu...Akahisi anapewa muda tu, dawa yake ipo jikoni yachemka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


MAPENZI HAYA[emoji23][emoji23]
 
Hufikiri, kusema na kufanya yasiwezekana
Watu wasioweza kufanikiwa hujaa fikra za kutofanikiwa na mara nyingi hulalamikia sana matatizo yao. Wakati mwingine wasioweza kufanikiwa hugeuza mambo mema na kuyafanya yaonekane mabaya, jua likiwaka watalalamika joto, likipoa watalaumu baridi, watalaumu foleni za barabarani, yaani kwao kila jambo wataligeuza na kulipa sababu mbaya. Hata wanaposhindwa kutekeleza jambo hutoa sababu, yote ni kuzilinda fikara zao za kutofanikiwa.
 
Tabia hii hukua mpaka kufikia hatua wanapowatazama wenzao hudhani kuwa wanawasengenya, kuwafanyia mambo mabaya, kuwasaliti, ilimradi tu ni kuwa kinyume na mambo mema. Watu wa namna hii hata kama watasaidiwa namna gani hugeuza misaada hiyo kuwa ya kujipendekeza na mara nyingi hupuuza wema haraka na kueneza mabaya ya mtu. Lakini pamoja na yote kutokana na fikra zao kuwa za kushindwa watu wa tabia hii hukata tamaa mapema, pale wanapofanya jambo na kuonekana lina ugumu kidogo.
 
Hutenda kabla ya kufikiri
Tabia ya pili ya watu wasioweza kufanikiwa kimaisha ni hii ya kutenda jambo kabla ya kufikiria. Watu wa aina hii, kuwa wepesi sana kununua vitu barabarani mara tu wanaposhawashiwa na macho au wauzaji. Utakuta mtu bila hata kujiuliza faida za kitu hicho anaamua haraka kukipata. Ataamua kwa haraka kuoa, kuolewa, kukubali kujiingiza katika mapenzi na hata kufanya jambo lo lote bila kujiuliza atanufaika vipi?
 
Hupenda kuzungumza zaidi ya kusikiliza
Watu ambao wako katika hatari ya kutofanikiwa ni wale ambao daima ni wazuri katika kuzungumza kuliko kusikiliza. Wao huwa ni wajuajia wa kila kitu, hawako tayari kupokea ushauri. Siku zote wanapokuwa kwenye makundi ya watu pengine wajuzi zaidi yao wao huwa hodari kujenga hoja kutetea mambo yao hata kama hayafai. Unaweza kumkuta mtu ni kiongozi wa ngazi za juu, amefanya kosa na watu wote wameona kuwa kakosea lakini mhusika hujiona si mikosaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…