Onyesha wazi kukubaliana au kutokukubaliana kwako na utoe sababu za kule kukubaliana au kutokubaliana
Jinsi gani ya kuwa mzungumzaji mwenye ujasiri
Kwa kule kuwa mzungumzaji mwenye ujasiri kunaupa nguvu ujumbe wako
Ujasiri wako katika kuzungumza huziteka hisia za msikilizaji/wasikilizaji wako kiurahisi
Usiruhusu kamwe mtu anayekusikiliza akaigundua ile hali ya wewe kutokuwa jasiri
Mambo ya kuzingatia ili kuwa mzungumzaji mwenye ujasiri
Jitahidi sana kutumia sentensi za “mimi” zaidi ya kutumia sentensi za “wewe”.
Wakati wowote mzungumzaji aliye jasiri ataielezea hali fulani akiihusisha na yeye na sio kukwepa au kujitetea. Kwamfano badala ya kusema “Najua wewe hunipendi ndio maana umenifanyia hivi” basi unaweza kusema “Mimi sifurahii vile unavyovifanyia.
Jitahidi na jifunze kutumia “sentensi” zaidi ya kutumia “maswali”.
Hii itaonyesha kuwa una ujasiri katika kile unachokizungumza na kwa wewe mwenyewe pia. Kwamfano, badala ya kusema “Hivi mnamwonaje boss wetu sikuhizi?” Unatakiwa kusema “Mimi sifurahishwi na tabia za boss wetu
Jitahidi kutumia sentensi za ukiri zaidi kuliko kutumia sentensi za lawama.
Sentensi za ukiri ni zile ambazo zinaelezea nini mzungumzaji angependa kuona kinafanyika au kinatokea, wakati kwa upande mwingine sentensi za lawama ni zile zinazoonyesha kile ambacho mzungumzaji hapendi kukiona. Kwa mfano, mtu kusema “Sipendi jinsi unavyonifanyia” hii ni sentensi ya lawama. Kwa upande mwingine mtu akisema “Ninatamani uwe na mtazamo mzuri juu yangu” hii ni sentensi ya ukiri.
Jifunze kutumia vema lugha ya mwili wako (body language)
Je unatumia mwili wako kwa namna gani au kwa kiwango gani katika kufikisha ujumbe? Kumbuka kwamba mwili wako waweza kuongea na kutuma ujumbe mkubwa sana pasipo hata kuzungumza kwa kinywa chako. Wataalamu wa mawasiliano wanasema kwamba zaidi ya asilimia 50 ya mawasiliano hufanyika nje ya mawasiliano ya kinywa (verbal) na hata nyakati tunapotumia vinywa vyetu zaidi ya asilimia 60 ya ujumbe hupenya kupitia maeneo mengine ukihusisha lugha ya mwili (non-verbal)
Maeneo haya ni kama vile muonekano wa uso wako (facial impression), namna ndita zako zilivyo au zinavyofanywa, macho yako, pua yako, au vile unavyouweka mwili wako (pose). Mara nyingine hata namna tunavyovaa huhusika pia.