Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama ambavyo giza halidumu milele na mitihani ya kimaisha pia haidumu milele hivyo ongeza mapambano na magumu, huzuni, changamoto ulizonazo zitapita pia, zitapitaje, zitakuacha katika hali gani, mwamuzi ni wewe.

Vivyo hivyo unapopata mafanikio pambana kuhakikisha yanadumu na kukua zaidi, badala ya kuyaacha yalipo au kukubali yapotee.
 
Kama ambavyo giza halidumu milele na mitihani ya kimaisha pia haidumu milele hivyo ongeza mapambano na magumu, huzuni, changamoto ulizonazo zitapita pia, zitapitaje, zitakuacha katika hali gani, mwamuzi ni wewe.

Vivyo hivyo unapopata mafanikio pambana kuhakikisha yanadumu na kukua zaidi, badala ya kuyaacha yalipo au kukubali yapotee.
 
Wakati wa mafanikio marafiki wa kweli na maadui marafiki huwa wengi, hapa ndipo busara, hekima, kukumbuka ulipotoka vinapohitajika.

Jifunze kwa waliofanikiwa, yafanyie kazi mawazo yao mazuri, huku ilichanganya na akili yako kuhakikisha unatimiza ndoto zako za mafanikio.

Wakati huu ujana huchukua nafasi kubwa, siku zote kumbuka usemi wa Wahenga usemao “Ujana Maji ya Moto” . Hivyo ukizubaa yatakuunguza muda wowote na hata kukujutisha hadi uzeeni.
 
Itumie vizuri nafasi ya kuchanua kwenye mafanikio badala ya kuchanganya mambo, kama unasoma, unafanya kazi, unalima, unafuga fanya hayo yite huku ukiwa na hofu ya kushindwa, kwa sababu kushindwa siyo sehemu ya malengo yako.

Zingatia malalamiko, lawama hayana nafasi katika safari hiyo ya mafanikio uliyoianza, usikubali kumtaja mtu mwingine kuwa chanzo cha wewe kushindwa.
 
Kwa sababu umeshatoka na umeanza safari ya mafanikio ushindi ndiyo njia sahihi unayotakiwa kupita. Piga hatua njia hiyo ipo karibu na hapo ulipo. Sina uhakika lakini kwa mtizamo njia hiyo ipo hatua chache kutoka hapo ulipo.
 
Itumie vema Leo yako, sahau kabisa kuhusu jana (imeshapita ukiikumbuka utaishia kulalamika), fikiria kuhusu kesho unayoijenga leo, usikubali leo ifanane na jana au ikupite wima. Furahia kupita kwenye matatizo kwa kuwa umeshayapatia ufumbuzi, jifunze vitu vipya. Kauli mbiu yako iwe mabadiliko, adui yako mkuu awe malalamiko.

Nikutakie safari njema ya mafanikio yaliyo hatua chache kutoka ulipo.
 
38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;

Mathayo 5 :38

39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.

Mathayo 5 :39

40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.

Mathayo 5 :40

41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.

Mathayo 5 :41

42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Mathayo 5 :42

43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

Mathayo 5 :43

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

Mathayo 5 :44

45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Mathayo 5 :45

46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

Mathayo 5 :46

47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

Mathayo 5 :47

48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…