Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

EDF6B1A5-B3ED-4ACA-9F71-07E03C365950.jpeg
 
.Watu wengi wamekuwa wakitafuta mafanikio maishani lakini tambua kwamba mafanikio ya kweli yatapatikana tu ukiwa na bidii, ustahimilivu, nidhamu pamoja na shauku kubwa ya kupata mafanikio. Zifuatazo ni mbinu tano muhimu zitakazo kusaidia kuwa mstahimilivu katika harakati za kutafuta maendeleo na mafanikio.
 
Fahamu matakwa yako.

Ninachomaanisha hapa ni kujua nini unataka, ukijua unachotaka utakuwa na msimamo wa kutaka kufikia malengo yako. Kama bado hujui nini unataka basi nakushauri ufanye hivi, chukua kalamu na karatasi kisha jiulize Unataka kufanikiwa kitu gani? Hapa ni muhimu wakati ukijiuliza unataka kufanikiwa nini basi ujitahidi kutofikiria mawazo hasi au mawazo mabaya ya kujiona kama utashindwa kufanikiwa. Jiamini, ondoa hofu au wasiwasi wowote utakaokuwa nao na orodhesha mambo yote unayotaka kufanikiwa katika karatasi yako na kisha anza kupanga mipango kwa kujiwekea malengo na kutekeleza moja baada ya jingine.
 
Nini kinakupa motisha au hamasa ya kutaka kufanikiwa.

Motisha ni chachu ya ustahimilivu kwani hukufanya kuendelea kushikamana na mipango yako mpaka mwisho licha ya kuwa na vipingamizi vingi katika njia yako ya mafanikio. Malengo mengine Ni ya muda mrefu hivyo yanakuhitaji uwe mvumilivu ili ufanikiwe, kama utakosa ustahimilivu wa kungojea matokeo unaweza kujikuta unakata tamaa mapema kabla ya kufikia malengo. Motisha ni kitu pekee kinachokusaidia kukusukuma uendelee kutaka kufanikiwa hivyo ni heri kila malengo unayojiwekea yawe ni yenye kukupa kiu ya kutaka kufanikiwa kwakuwa unapenda hayo unayohangaikia.
 
Back
Top Bottom