Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tunaenda kuona tumboni kwa huyu kiumbe kuna nini hasa[emoji3] [emoji3] [emoji3]
FB_IMG_1530631974714.jpg
 
Isaya 59:1

Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;

Isaya 62:6

Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;

Isaya 43:26

Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Mithali 8:17

Nawapenda wale wanipendao,Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

Isaya 55:6

Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,Mwiteni, maadamu yu karibu.
 
Usingizi ni moja kati ya vitu muhmu kwa afya ya binadamu. Kukosa usingizi ipasavyo (masaa 6-8) hupelekea matatizo kama uchovu siku inayofuata, kusinzia siku inayofuata, kupungua uzito, kupungua kinga ya mwili n.k. Kuna imani potofu ya kwamba watoto ndio wanaopaswa tuu kulala muda fasaha.
 
Kwa kuwa watu wengi hawapo makini katika kuangalia mienendo ya maisha yao, hawawezi kujua sababu zinazopelekea matatizo hayo, hivyo kukosa sululuhu ya kudumu. Zifuatazo ni sababu zinazopekea ukosefu wa usingizi, baada ya kuzijua itakuwa rahisi kwa mtu kukabiliana na changamoto.
 
Kula chakula kingi muda mchache kabla ya kulala.

Kula chakula kingi, hususani nafaka, muda mfupi kabla ya kulala hufanya mwili utumie nishati nyingi katika kumeng'enya chakula, hivyo kuvuruga utaratibu wa nishati wa mwili. Pia kunywa maji kabla ya kulala humfanya kuamka usiku ili kujisaidia, hivyo kubadili utaratibu wa usingizi.
Mtu anapaswa kula chakula chepesi na maji kidogo angalau nusu saa kabla ya kulala.
 
Kulala mazingira duni.

Kulala katika mazingira yanayokinzana na utu wa mtu huvuruga utaratibu wa mwili. Mazingira kama; chumba chenye mwanga mkali, chumba chenye joto au baridi kali, kulala kwenye kelele, kulala kwenye godoro laini au gumu sana, chumba kisicho na hewa safi ya kutosha n.k humfanya mtu kukosa usingizi.
 
Back
Top Bottom