Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kubadili mfumo wa maisha.

Kubadili mfumo wa maisha na ambao ulikuwa umezoelewa na mwili hutatiza usingizi. Kwa mfano; kumpoteza ndugu au rafiki wa karibu, kuanza kazi mpya, kufanya kazi ngumu, kuingia kwenye ndoa, kuwa na msongo mawazo n.k huwafanya watu wengi kukosa usingizi.
Hali hii huchukua siku chache, ikiwa kama ukosefu wa usingizi itachukua muda mrefu, mtu anapaswa kufanya tahtmini ya kina.
 
Mazingira duni ya kijamii.

Mazingira duni ya kijamii kama; kulala zaidi ya mtu mmoja kwenye kitanda kimoja, kulala na mtu msumbufu hususani mtoto mdogo, kulala chumba kimoja na mtu anayekoroma, kulala na mtu anayesumbua usiku, kulala chumba chenye wadudu kama chawa, kunguni, viroboto n.k.
Mazingira haya yanasababishwa na umasikini wa kipato.
 
Matumizi ya madawa.

Kuna aina nyingi sana ya madawa ya hosptalini ambayo, pamoja na kutibu au kupunguza maumivu, hupelekea kukosekana kwa usingizi. Madawa hayo ni kama madawa ya kupunguza maumivu, kupunguza mawazo, madawa ya usingizi n.k.
Mtu anapaswa kusoma maelekezo au kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa yoyote ile ili apate kujua madhara yake na jinsi ya kuyakabili.
 
Matumizi ya vinywaji baridi na sigara muda mchache kabla ya kulala.

Vinywaji baridi vina kokaini, chai au kahawa ambayo huongeza msukumo wa damu. Matumizi ya vinywaji hivyo kabla ya kulala kukatiza usingizi. Kwa upande wa sigara, ikilinganishwa na watu wasiovuta sigara, watu wanaovuta sigara hukawia kupata usingizi, hivyo, kupata masaa machache ya kulala.
Kuna watu wamezoea kunywa pombe ndipo wapate usingizi, watu hawa ni watumwa wa pombe na wengi wao hutumia pombe kali, baada ya muda, pombe haitoweza kumsabishia usingizi kabiasa au akiwa hana hela ya kununua pombe mtu huyo hatoweza kulala.
 
Kwa kiasi kikubwa, sababu za ukosefu wa usingizi zipo chini ya uwezo wa binadamu, hivyo, mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla inapaswa kutengeneza mazingira yanayopekekea usingizi murua, mafanikio ya mtu katika kazi za kujiletea maendeleo, hutegemea, pamoja na mambo mengine, kiasi cha mapumziko anayopata kila siku kupitia usingizi.
 
**UNAWEZA UKASEMA, MIMI SIJALI WATU WANASEMA NINI JUU YANGU....LAKINI NAKUHAKIKISHIA, JARIBU KUJALI.**

Naam! Katika Maisha haya, tumeumbwa wengi,kila mmoja akiwa na makusudi yake,lakini tukiwa tunafaana na kuhitajiana kwa namna moja ama nyingine!
Kila siku unahitaji watu,na nikisema watu,simaanishi unaowajua au mnaojuana, ila watu kama watu tu!

Ukitoka nyumbani unahitaji wa kumwacha nyumbani; Ukiwa na nyumba kubwa unahitaji wa kukufungulia geti; ikiwa unatumia usafiri wa wote, basi unahitaji mtu mwenye pikipiki bajaji au daladala ili akufikishe uendako! Hata kama una gari yako,kuna mahali utamwitaji askari wa barabarani ili akusaidie dhidi ya foleni!
Unahitaji kujua yanayoendelea, kwahiyo unamwitaji mtangazaji au mwandishi! Huko mchana unaweza kuhitaji maji au chakula,kwahiyo pia unawahitaji watu!
Na idadi inaenda hivyo week hata mbali sana!
Yaani hata maiti inahitaji watu wa kuizika.
 
Watu wanayo maoni mengi sana juu yako! Mengine wanasema kwako mengine wanasema kimoyo moyo na mengine wanaambiana wao kwa wao!
Ni wazi kuwa yale mazuri yatakufurahisha na yale yenye ukakasi yatakukalaisha!
Lakini ukweli unao wewe mwenyewe!

Wanasema usijali watu wanasema nini juu yako, Ooh wasipokupenda, asipokuwepo rafiki wa ukweli ila rafiki akupendaye akiwa ni Yesu yatosha!
Ni vizuri kuwaza hivyo ukiwa mnyofu na ukiwa na picha njema ya kesho yako!
Na ni nzuri kwa kujifanya huoni mambo ya msingi!
Ila Ukweli ni kuwa, kwa namna yoyote ile unatakiwa kujali watu wasemayo!

Sio lazima kujali sana wala kujali yote,lakini hata kama ni kidogo au kwa mbali,muhimu sana kujali maoni ya watu juu yako!
Wewe hujioni, hao ndio wanakuona!
Lakini pia wewe huishi kwa ajili yako ila unaishi kwa ajili ya wengine!
Inawezekana mtazamo na maoni ya wengine yakawa hasi kwasababu ya ukakasi ulio ndani yao wenyewe au hasira tu au chuki tu lakini kutokuelewa sawasawa!
Kwa hali kama hiyo unaweza kupuuzia na kuwapa muda,yamkini kesho na kesho kutwa wakaelewa!
 
Waterspouts are a whirling column of air and mist. According to the National Ocean Service, waterspouts fall into two categories; fair weather and tornadic. Fair weather waterspouts develop on the surface of the water in light wind conditions and work their way upward with little movement. The more volatile tornadic waterspouts share the same characteristics as land tornadoes and are typically associated with thunderstorms including high winds and lightning. Tornadic waterspouts are tornadoes that form over water or have moved from land to water. When waterspouts move to land, the National Weather Service issues a tornado warning.

 
Lakini ukiona Maoni ya wengi yanasema kitu kile kile juu yako, usiseme tu "i don't care", chunguza uone, Usijifukie! Yamkini kuna mambo unahitaji kurekebisha na kuweka sawa!
Kila mmoja anasemwa hapa na pale, lakini kwanini wewe usemwe,hapa na pale huku na kule na kule tena,tena sana na mbaya zaidi kwa mabaya tu!

Usitafute kimvuli cha kuficha uchafu na Upumbavu wako kwa kusema, Hata waseme nini,mimi sijali!
Kuna kiwango cha kupuuzia maneno ya watu, lakini Usipuuzie kabisaaa!
Yesu mwenyewe, alifika wakati akawauliza wanafunzi wake "Eti watu Wanasemaje kuhusu mimi?" kimsingi alikuwa anatafuta kujua kama ameeleweka kwa kiasi gani? Lakini hawa wamesikia kwa kiasi gani! Na walimpa majibu!
Kile walimwambia,walikuwa wamesikia siku nyingi au mara nyingi na hawakusema mpaka ameuliza! Kwahiyo nawewe unayo nafasi wakati mwingine kujiuliza au kutafakari yale watu wanasema juu yako na yanajirudia rudia!

Ni wazi kuwa ukisema, Mimi sijali Unajali sana na ndio maana ukasema hayo!
Na wanaokuunga mkono ni kama wewe au wana hali mbaya zaidi yako ya kiburi!
 
Kuna maneno ni ya kupuuzia,mfano mtu anasema hujui kuvaa,yamkini ni mtazamo wake,ingawa unatakiwa kuzingatia Viwango na wewe; au hujui kucheza au Umepotea hali unajiona upo au mtu anakwambia pale huwezi kufanikiwa,kisa yeye alishindwa,hayo sio muhimu sana!
Lakini ukisikia watu wanasema wewe ni Mdungunyuaji(Malaya), ni wazi kuwa maneno hayo hayawezi kutokea hewani tu!
Ukisikia watu wanasema una kiburi, hiyo sio ya kupuuzia,ni dalili mbaya sana!
Na hasa ukiwa Kiongozi au Mtumishi wa Mungu, chunga sana hiyo!
Ukiambiwa wewe dhulumati au Muongo,Jitafute na urekebishe, usiseme tu, Mimi sijali!

Kwahiyo ni muhimu sana sana kutokujali maneno na maoni ya watu baada ya kujali na kujiridhisha kuwa hayo sio ya kujali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…