Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

D347AC03-EF89-4E60-A46B-DD444FBDDFB3.jpeg
 
Kwa mtu kuamua kuwaza juu ya kifo chake ni jambo zuri, tafiti zimethibitisha hivyo tofauti na mitizamo ya watu.
Watu wengi huogopa sana pindi wanapoona jeneza au kupita makaburini au kusikia juu ya msiba. Hivyo kujikuta wakitafakari juu ya maisha yao.
Kifo kinatisha kwa kweli, maana inakuwaje kila anayekufa anapitia machungu ya ugonjwa au ajali. Na mara nyingi anayekufa lazima akojoe na au kumwaga haja kubwa. Kwa kweli nikitafakari hapo hukiohopa sana kifo. Ni vile siri yake haijulikani mpaka kikufike.
Mwenyezi Mungu atuepushe na kifo chenye machungu. Aamin
 
Kuna baadhi ya mitizamo hasi ya kwamba mtu anayetafakari juu ya hatima yake, na kuongea hakawii muda mrefu bila ya kufariki. Baadhi ya watu huenda mbali zaidi na kusema ya kwamba mtu anayekaribia kufa huona baadhi ya dalili ndani ya siku arobaini kabla ya kifo chake, hivyo kumfanya aongelee kufa.
Kifo ni lazima tukitafakari. Na ukikitafakari sana lazima umche Mola wako, maana kuna siri kubwa hapo
 
b) Kusaidia kuimarisha afya.

Watu hukata shauri na kwenda hosptali au vituo vya afya ili kupata kuchunguzwa afya zao (mfano kupima VVU, malaria n.k) baada ya kuambiwa madhara ya matendo yao au hatari zinazowasonga, kiasi cha kutishia uhai wao.

Pia watu huchukua tahadhari kama kufanya mazoezi, kubadili mfumo wa vyakula n.k ili kupunguza uwezekano wa kupata matatizo kama shinikizo la damu, kisukari n.k.
Ni kweli
 
Kila nafsi itaonja mauti! Hivyo kila mtu anapaswa kutafakazi, je matendo yake yanashabihiana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu?

Wakati wa kurudi kwa Muumba hakuna nafasi ya kubeba hata sehemu kidogo ya mali mtu alizozalisha au kwa mabavu au kwa njia njema. Kila mtu anapaswa kuwa mfumo wake wa maisha utakaodumu hata baada ya kifo chake. Kwani mtu hufa lakini matendo na mwenendo wake mwema humweka hai na kubaki kama ua katika jamii alimoishi.
Sahihi kabisa. kaburini hatutaenda na magari wala majumba. Ni amali pekee, ima iliyo njema ama mbaya kadiri ya maisha uliyoishi duniani
 
Kwa jam, watu wa magari kubwa kama v8 na range rover wanauziwa property magazine [emoji849]
Watu wa gari ndogo kama premio na NZE wanauziwa mandizi, jumper cables na alphabetical charts [emoji12]
Sisi Watu wa matatu tunauziwa dawa ya mende, kunguni, minyoo na mitego ya panya ........
Sawa tu "bora uhai"
 
Back
Top Bottom