Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ufanisi wa bajeti ukazikwa na Upimaji wa samaki bungeni,upimaji wa Samaki ukazikwa na korosho,Ya Korosho yakazikwa na ya Mwigulu,Ya Mwigulu yalizikwa na ya wastaafu kwenda kuzungumza na Mh Rais,Ya wastaafu kwenda kumuona Rais yakazikwa na ripoti ya Twaweza,ripoti ya Twaweza ikazikwa na tukio la waziri Kangi kumfurushwa kamishna wa magereza.
 
1.Man City – wachezaji 11
Benjamin Mendy (Ufaransa), Gabriel Jesus (Brazil), Danilo (Brazil), Fernandinho (Brazil), Ederson (Brazil), Vincent Kompany (Ubelgiji), Kevin De Bruyne (Ubelgiji), Kyle Walker (England), John Stones (England), Raheem Sterling (England) na Fabian Delph (England)
Arsenal ina wangapi[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Uongozi ama leadership unaelekeza mpaka namna ya kushughulika na viongozi wenzako hasa unapobaini kiongozi mwenzako kakosea na kosa limefanyika sehemu ambayo kuna watu anaowaongoza.

Basi tukaambiwa,kwenye masuala ya Uongozi huwa kuna vikao vya ndani vya kuonyana wenyewe kwa wenyewe.
 
Wazee waliokutana na Mh Rais John Magufuli,kuna mambo waliyazungumza na yana mantiki kubwa.Hebu tuyatafakari

1."Mimi ningependa kusikia zaidi,Serikali yetu inajitambulisha zaidi kama serikali ya CCM,na hasa mawaziri,maana ,hii ni serikali ya CCM inaongozwa na Rais Magufuli,lakini nae ametokana na CCM,hii ya kusema mimi,mimi,aaaa,aaa"
Benjamini Mkapa...

Mtazamo: Nadhani hii inatokana na baadhi ya viongozi wawapo kazini huishia kusema,Serikali ya Magufuli .....badala ya Serikali ya CCM,ukitazama unaona Viongozi wanauza "image" ya Rais zaidi kuliko ya chama,na inaonekana haya yanafanywa na Rais na siyo Chama.

2." Naunga mkono alilolisema Jaji mkuu mstaafu Augustino Ramadhani kuhusu utawala wa sheria,juhudi zote zinzofanyika,kwenye uchumi na kwenye sehemu nyingine ni lazima ziwe ndani ya utawala wa sheria,nadhani lazima tukubaliane katika hilo,na utawala wa sheria lazima uambatane na haki,bila haki,hakuna utawala wa sheria,na unaweza kuwa na sheria lakini zikawa mbovu,wakati mwingine naposikiliza TV nakuona kauli za baadhi ya viongozi wetu hasa ma DC nabaki najiuliza hivi sheria ipo wapi?".Jaji mkuu mstaafu Barnabasi Samata.

Mtazamo:Nadhani hii inatokana na tabia ya baadhi ya viongozi wetu kusema,kwenye suala la maendeleo sheria tuziweke pembeni,sasa wapo baadhi ya viongozi wameweka pembeni sheria kwa kisingizio cha maendeleo.

3."Amani ni tunda la haki,kama hakutakuwa na haki,basi hakuta kuwa na amani,kama haki itatetereka basi hapo kutakuwa na wasiwasi wa amani.Mh Rais,tuje kwa mawaziri,tuje kwa RC,tuje kwa ma DC,tutekeleze haki".Jaji mkuu mstaafu Augustino Ramdhani.

Mtazamo:Nadhani hii inatokana na baadhi ya watu kudhani suala la amani halina msingi wake,wanadhani amani ipo tu bula kujua amani ni msingi wa haki.

4."Kila wakati isiwe watu wanamrefer Rais,sijui Rais kasema,Rais Kasema,kwani nayeye ni mtu,badala ya kusema Raisi kasema,kuna general orders,ziandikwe siyo lazima kujenga kitu kipya lakini vitu mnavyofikiri ni vipya viingizwe humo kwenye general orders badala ya kila jambo kusema,Rais,Kasema,Rais kasema"Mh Spika mstaafu Anne Makinda.

Mtazamo:Nadhani hii inatokana na baadhi ya viongozi wetu,badala ya kunukuu sera,sheria,mwongozo na taratibu wanapotekeleza wajibu wao,utawasikia wanasema,"Mh Rais ameshasema,"badala ya kusema,sheria inasema,ama sera inaelekeza.

5."Tunasema maneno mengi ambayo hatuyapimi ,kama yanaweza kutuondolea amani tuliyonayo,amani tuliyonayo ni muhimu sana,Mwalimu Nyerere alipata kusema,ukitaka kupima nchi yenye amani na Demokrasia,hesabu viongozi wake waliopo nje" Edward Lowasa.

Mtazamo:Nadhani hii inatokana na tabia ambayo imeaanza kujengeka watu kutoa kauli nzito bila kupima kama zina afya ama lah,kwa ustawi wa nchi yetu.

6."Kama watu watakumbuka wakati nakwenda upinzani,nilisema sina chuki na CCM,sina chuki na Rais Magufuli,sina chuki na Rais Kikwete,lakini nilisema nakwenda upinzani kwa maslahi ya nchi hii,na kwa wale wanaokumbuka nikasema,kwenda kwangu huko itakuwa ni kwa faida pia ya CCM" Fredrick Sumaye.

Mtazamo:Nadhani hii ni kutokana na baadhi ya watu kujiuliza hivi inawezekana vipi Sumaye aliyekuwa mpaka waziri mkuu kwa miaka kumi na wakati alipokuwa CCM aliwahi kutoka misimamo mikali,lakini akatoka na kwenda Chadema?
 
This is Cristiano Ronaldo one of the richest sportsman in the world with his girlfriend...

They're out on a treat & with them on the table are 2 glass cups of wine only....

Ladies, food is not everything

DhfptwdW4AEAvBC.jpg
 
Back
Top Bottom