Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

LA LIGA

Kwenye Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, Barcelona ndiyo yenye wachezaji wengi waliotinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia huko Russia ikiwa nao wanne; Samuel Umtiti, Ousmane Dembele, Ivan Rakitic na Thomas Vermaelen wakati Real Madrid inao watatu; Raphael Varane, Mateo Kovacic na Luka Modric.
 
Atletico Madrid ina wachezaji watatu pia; Lucas Hernandez, Antoine Griezmann na Sime Vrsaljko huku staa wao wa nne, Thomas Lemar alianza michuano hiyo akiwa bado mchezaji wa Monaco.
 
LIGUE 1

Kwenye Ligi Kuu Ufaransa, mabingwa wa Paris Saint Germain wana wachezaji wanne ambao ni Alphonse Areola, Presnel Kimpembe, Kylian Mbappe na Thomas Meunier. AS Monaco inao wanne pia; Djibril Sidibe, Thomas Lemar, Danijel Subasic na Youri Tielemans huku Olympique Marseille ikiwa na wachezaji watatu tu, Steve Mandanda, Adil Rami na Florian Thauvin.
 
BUNDESLIGA

Kwenye Ligi Kuu Ujerumani hakuna timu yenye mchezaji zaidi ya mmoja, kwani klabu za kwenye ligi hiyo zina mchezaji mmoja mmoja waliofanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.
 
Klabu hizo ni Bayern Munich (Corentin Tolisso), Stuttgart (Benjamin Pavard), Bayer Leverkusen (Tin Jedvaj), Hoffenheim (Andrej Kramaric), Eintracht Francfort (Ante Rebic), Schalke 04 (Marko Pjaca), Wolfsburg (Koen Casteels), Borussia Monchengladbach (Thorgan Hazard) na Borussia Dortmund (Michy Batshuayi).
 
Back
Top Bottom