Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Imeripotiwa kuwa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama pamoja na familia yake wamewasili nchini Tanzania kimyakimya Jumapili Julai 8 kwa ajili ya mapumziko ambapo imeelezwa watatumia muda wa wiki moja kushuhudia vivutio mbalimbali vya utalii nchini.

Kwa sasa Obama na familia yake wako katika hifadhi ya taifa ya Serengeti

[emoji991] kwa hisani ya mitandao
 
HUYU NDIYE MTANZANIA ALIYESHIRIKI UUNDWAJI WA NDEGE MPYA YA DREAMLINER: Mtanzania George Jonas ndiye Mhandisi wa umeme aliyekuwa na jukumu la kuangalia mfumo wa kiusalama wa umeme katika ndege mpya ya Dreamliner.

Anafanya kazi katika Makao Mkuu ya Kampuni ya Boeing Settle ,Washington, Marekani.

George Jonas ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya na ndiye aliyekuwa miongoni mwa maafisa wa kiufundi aliyehusika katika utengenezaji wa ndege hiyo yenye viti 262, kwa jina Boeing 787-8 Dreamline.

Mhandisi George ni mtoto wa mwanajeshi mstaafu, Labani Mwanjisya ambaye safari yake ya masomo ilianzia pale Shule ya msingi Ubungo na baadaye kuendelea na elimu ya Sekondari Azania na kisha alijiunga na elimu ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Ilboru ambapo alichukua masomo ya Fizikia, Chemia na Hisabati.

Mara baada ya kuhitimu masomo yake ya kidato cha sita alibahatika kupata fursa ya kwenda Marekani kwa masomo zaidi baada ya kundi moja la Wamarekani waliokuwa wakitafuta kijana wa Kitanzania mwenye maono kumchagua yeye.

Mwenyewe anasema, ilikuwa kama bahati kwake kwani kwa wakati huo wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumpeleka masomoni ughaibuni.
 
kenewest.jpg
 
Back
Top Bottom