Paulo Dybala
Kocha wa Argentina, Jorge Sampaoli hakutaka kabisa kumpa nafasi Paulo Dybala kwenye kikosi chake katika fainali za Kombe la Dunia huko Russia.
Staa huyo aliishia kukaa benchi tu muda mwingi wa fainali hizo licha ya kuorodheshwa kwenye moja ya wachezaji ambao wangekuwa tishio zaidi katika fainali hizo kama wangepewa nafasi. Kwenye kikosi cha Juventus, Dybala alikuwa mmoja wa mastaa wa maana, hivyo iliwashangaza wengi kuona Argentina inashindwa kumtumia vyema na matokeo yake walikomea kwenye hatua ya 16 bora tu kwenye fainali hizo, wakati walipochapwa na Ufaransa. Dybala ni mmoja wa wachezaji wanaotajwatajwa huko Bernabeu huenda wakapewa nafasi ya kwenda kuziba pengo la Ronaldo, ambaye amekwenda Juventus. Lakini, shida inakuja sehemu moja, Juventus watakubali Dybala aondoke?