Katika kitabu kigumu kabisa kukieliwa hapa duniani ni Biblia, na katika kitabu kirahisi kabisa kukielewa hapa duniani ni Biblia.
Neno "kufa" katika biblia hutajwa mara 307, Neno "kupenda" katika biblia hutajwa mara 306, neno "kwapamoja" katika biblia hutajwa mara 246, neno "usiogope hutajwa mara 365 katika biblia.....
Unajua kwanini neno "kufa" limetajwa mara nyingi, na kwanini neno "usiogope" limetajwa mara nyingi zaidi kuliko neno lolote? Haya endelea kuwa wajinga sawa na mjinga mkuu mie, ujinga sio ulemavu ni mapito tu kuelekea uelevuni, Viwanda vimepunguza uzalishaji, wafanya kazi wamepunguzwa, maduka makubwa huko na kwingine yamefungwa, Wafanyabiashara wengi wanahamisha mitaji yao kwenda kwingineko,
Hali ni mbaya, pesa imekata mtaani, kazi hakuna, tunaishi mlo mmoja, Gesti na hoteli hazijai tena, badala yake Wodi za wagonjwa wa Presha na bodaboda zimejaa. Ukimuuliza spika wa bunge la Bosnia na Herzegovina na naibu wake kuwa pale bungeni huwa wanawakomoa wapinzani au taifa? Leo watakosa jibu.......
Mungu hulaani taifa lake lolote linalomtweza, na kwa hakika laana tuliyopewa na Mungu ni kutawaliwa. Mpaka siku Mungu ajiridhishe wajinga wote wameisha... Ndipo atamchagua mmoja wetu kati ya wenye akili ndipo atuokoe, lakini hii si rai ya nyie kufunga vinywa vyenu mkisubiri maagano ya Muumba wenu, laa hasha, sauti zenu zitasikika mkipanua vinjwa na akili zenu!
Mungu ni imani, na imani yako itakuponya, Mungu wa Yericko sio Mungu wa Malisa GJ, na Mungu wa Tanzania sio Mungu wa Marekani. Ndio, yanini Mungu mmoja atugawe katika makundi haya ya wenye nacho na wasio nacho, ya walala heri na walala hoi, ya mfupi na mrefu nk? Ndio kwa hakika imani zetu ni haba kama punje ya haradari.... Walau tungekuwa na imani hata ndogo tu angalau ya punje ya haradili, tungekataa kutawaliwa na tungechagua kuongozwa....
Acheni nitambike mie kwa imani yangu... Wote natuseme.... Tawireeeee!!!!
Moyo wa mtu ni msitu mnene!
Na Yericko Nyerere