Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1531847691405.jpg
 
Rais wa Lyon, Jean Michael Aulas amesema bado Liverpool wanaweza kumsajili kiungo wake Nabil Fekir msimu huu, pamoja na uhamisho huo pauni 53 milioni kuvunjika kutokana na Kombe la Dunia.

Uhamisho huo ulifikia katika makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka mitano na mchezaji huyo kutegewa mshahara wa pauni140,000 kwa wiki baada ya kubaliano ya mchezaji na klabu.
 
Hata hivyo haikufanikiwa baada ya kushindikana kwa kufanywa vipimo vya afya walivyotaka Liverpool, lakini sasa rais wa Lyon, Aulas amekiri kila kitu kinaweza kwenda sawa kama ilivyokuwa.

'Nafikiri mimi na Liverpool tunaweza kurudi katika meza ya mazungumzo,' Aulas alisema kipao mbele ilikuwa ni Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia.
 
'Uhamisho wake ulishindikana Juni, lakini haikuhathiri kitu. Akili yake ilikuwa Kombe la Dunia, nab ado moyo wake upo Lyon.

'Labda anaweza kwenda Liverpool, au klabu nyingine, lakini kama atabaki Lyon itakuwa ni mwaka mzuri kwake na kwetu pia.'
 
HII inaitwa hakuna kulala. Jose Mourinho ametoa wiki tatu tu za mapumziko kwa wachezaji wake waliotoka kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia na baada ya hapo warudi mzigoni huko Manchester United haraka.

Wachezaji saba wa Man United wamehusika kwenye mechi za Kombe la Dunia 2018 za wikiendi ya mwisho kabisa, ambayo ni juzi Jumamosi na jana Jumapili, lakini Kocha Mourinho amewataka warudi Old Trafford hadi kufikia Agosti 6.
 
Kuna mpango wa kuwaanzishia benchi wachezaji hao katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England, Man United itakayomenyana na Leicester City, Agosti 10.

Jesse Lingard, Ashley Young, Marcus Rashford na Phil Jones waliokuwa kwenye kikosi cha England, wakati Romelu Lukaku na Marouane Fellaini walikuwa na kikosi cha Ubelgiji na Paul Pogba alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa ambapo wachezaji hao walikuwapo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 iliyomalizika jana.
 
Ufaransa ilimenyana na Croatia katika mechi ya fainali. Wachezaji wengine wa Man United waliokuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia ni Marcos Rojo, David de Gea, Nemanja Matic, Victor Lindelof na Fred, ambao itakuwa hatihati kucheza kwenye mechi hiyo ya kwanza ya msimu kwenye Ligi Kuu England.
 
Back
Top Bottom