Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini wachezaji hao wote wamepewa mapumziko ya wiki tatu, ambazo zitawafanya wasiwepo kwenye ziara ya Marekani, lakini watapaswa kujiunga kikosini Agosti 6, siku nne tu kabla ya kucheza mechi yao ya kwanza kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City, Ijumaa, Agosti 10.
 
Man United itazindua ziara yake ya Marekani kwa mechi dhidi ya Club America mjini Phoenix, Ijumaa hii.

Baada ya hapo itakipiga na San Jose Earthquakes Jumapili kisha itafuatiwa na mechi dhidi ya vigogo AC Milan, Liverpool na Real Madrid.
 
Man united wangefanikiwa kumsajiri Mbappe na kumbakisha Pogba wangefanya jambo kubwa kuliko wanavyotaka kufanya
 
Maafisa nchini Urusi wamewafunguliwa mashtaka wanachama wanne wa kundi la Pussy Riot kwa kuvuruga mechi ya fainali walipoingia uwanjani mechi ya fainali ikiendelea.
Wameshutumiwa kwa kukiuka sheria zilizowekwa kwa mashabiki katika mashindano pamoja na kuvaa sare za polisi kinyume na sheria.
Makosa hayo yanavutia faini ya kati ya pauni (£121 na $161) yaani pesa za Urusi roubles 10,000 na 1,500, mtawalia.
Pussy Riot imejitetea kuwa maandamano yao yalikuwa yanapinga ukiukaji wa haki za kibinadam Urusi.
Walinzi wa usalama waliwachuja kutoka uwanjani.
 
Tukio hilo lilikatiza kipindi cha pili mechi ya fainali kati ya Ufaransa na Croatia na kusitisha mechi kwa takriban sekunde 25.
Ufaransa ilijinyakulia ushindi wa 4-2.
Usalama ulikuwa ni wa hali ya juu na haifahamiki jinsi wanaharakati hao walivyoingia uwanjani namna gani.
Pussy Riot wamewahi kuandaa maandamano ya hali ya juu dhidi ya rais Vladimir Putin hapo awali.
 
Wanachama wake watatu walikamatwa mnamo 2012 kwa kutunga wimbo dhidi ya Rais Putin ulioandaliwa jengo la kanisa kuu la Moscow.
Kundi hilo limeeleza kuwa wanachama wake waliokamatwa Jumapili walimaliza usiku kucha ndani ya kituo cha polisi katika hali mbaya na watafikihswa mahakamani kuhukumiwa kwa "makosa ya usimamizi".
 
Hisia mseto
Wanawake watatu na mwanamume mmoja walikimbia kuingia uwanjani,ingawa mmoja wao alipigwa rafu na kutofanikiwa kuingia. Walivaa sare zilizofanana na za maafisa wa polisi: Shati nyeupe, suruali nyeusi na madaraka.
 
Baada ya hapo, Lovren aliwaambia waandishi: "Nilizidiwa na hisia na kumkaba jamaa huyo na natamani ningekuwa na uwezo wa kumrusha hadi nje ya uwanja."
Beki Lovren alimkamata, mmoja wa waharibifu hao.
Mtu huyo alitajwa kuwa Pyotr Verzilov, mumewe Nadezhda Tolokonnikova, mmoja wa wanaharakati watatu wa kundi hilo la Pussy Riot waliokamatwa 2012.
Wanawake hao wametambuliwa kuwa Nika Nikulshina, Olga Kurachyova na Olga Pakhtusova.
Kulingana na taarifa kutoka kwa kundi hilo Pussy Riot, wamejitetea kuwa lengo la tendo lao lilikuwa ni la kutoa ujumbe kwa mamlaka za Urusi:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…