Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Uchapishaji cha Five Star, Ashikabbas Karim(30) maarufu kama Shakirali na wafanyakazi wake wanne, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka tisa, likiwamo la kuajiri raia wa kigeni ambao hawana vibali vya kazi.
Mbali na Karim, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 231 ya mwaka 2018 ni Aroygam Mocharias (38), (mwendeshaji) Mahesh Goud( 32) maarufu kama Budige,(Msimamizi wa Uzalishaji) HarishRaju Poojary(35) maarufu kama Bangeara, (Msimamizi) na Kiran Kumar(30) maarufu kama Koneti (Fundi) wote raia wa India na wakazi wa Vingunguti, jijini hapa.