myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Likes zinaendelea kutolewa
AiseeeUkistaajabu ya Musa!! Pichani juu ni waliaji wa kukodishwa kwenye misiba(professional mourners) wa S.Africa. Gharama zao kulia misibani ni: . 1.kulia kawaida gharama kwa kila mliaji ni R200 sawa na elfu 6500 za Tz . 2.kilio cha kujigalagaza chini kwa kila mliaji gharama ni R300 sawa na elfu 9500 za Tz . 3.kilio cha uchungu na kutukana kidogo matusi ya hapa na pale kwa kila mliaji gharama ni R400 sawa na elfu 13000 za Tz . 4.kilio cha uchungu na kutishia kujirusha kaburini kwa kila mliaji gharama ni R500 sawa na elfu 16500 za TZ . Kwahiyo wenye msiba huweza kugharamia kilio single au vilio mseto. Pia huduma zao huzingatia makubaliano ya muda. . Mliaji mwanaume mzungu wa Uingereza anasema biashara ya uliaji(crying business) kwenye misiba imeanza kuwa na ushindani mkali sababu za waliaji chipukizi kuanza kuibuka. . Amesema changamoto nyingine ni waliaji wapya mamluki wasio na skills nzuri kwenye business hiyo hivyo kutishia uaminifu wao wa kutoa huduma bora kwa wenye misiba. ameongeza kuwa kampuni zilizo kwenye business hiyo zimeanza kufanya auditions(usaili) na kutoa training(mafunzo) kwa waliaji wao ili wahimili ushindani sokoni . Kampuni ya Uingereza na Dallas, Marekani pia zinatoa huduma ya kujaza waombolezaji wa kukodishwa kwenye misiba. wanasema wanapata wateja sababu sifa kuu ya msiba ni vilio na huzuni hivyo wahusika waliopatwa na misiba wanapokosa waombolezaji wa kutosha na waliaji hujishtukia na kujisikia aibu ndio maana wao wanatoa kiki za kulia misibani mambo yaende vizuri . Anasema yeye Kama mliaji aliyebobea(professional mourner) sababu ya ushindani uliojitokeza inamlazimu kabla ya kuanza kutoa huduma kwenye msiba kuanza kufanya research(utafiti) kwanza ikiwemo kukaa karibu na ndugu au marafiki wa aliyeaga dunia ili kuuvaa uhalisia asije kuharibu kwa waomboeazaji kibarua kikaota nyasi kukosa michongo siku za usoni . Anasisitiza kuwa mfano katika kujiongezea ujuzi zaidi kabla ya kwenda kwenye tukio waliaji wanawake anaowajua hukumbuka misiba ya ndugu zao iliyowahi kuwakumba au hutazama movies za kuhuzunisha ikiwemo Titanic ili kukabiliana na changamoto na ushindani wa kiwanda cha uliaji(crying industry).View attachment 817586
AminAmani na upendo udumu