Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23]
20180724_212316.jpg
 
Mshambuliaji Harry Kane na Mohamed Salah wametajwa katika orodha ya wachezaji kumi wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Fifia 2018, huku Neymar akiachwa.

Nahodha wa England, Kane na nyota wa Liverpool, Salah wametaja katika orodha ya fifa iliyotolewa leo Jumanne ya wachezaji hao 10, waliopitishwa na jopo la na wachezaji wa zamani wenye mafanikio makubwa kama Kaka, Didier Drogba na Frank Lampard, na wengine.
 
Bingwa wa Kombe la Dunia Ufaransa, ametoa wachezaji watatu katika orodha hiyo Antoine Griezmann, Kylian Mbappe na beki Raphael Varane pamoja mshindi wa mpira wa dhahabu Luka Modric.

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard pamoja na kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne wameungana na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika kinyang’anyiro hicho.
 
Hata hivyo, hakukuwa na nafasi Neymar, pamoja na Mbrazil huyo kufunga mabao 28, katika msimu wake wa kwanza Paris Saint-Germain.

Neymar alishindwa kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya Brazil kuchapwa na Ubelgiji.
 
Baada ya orodha hiyo kutoka manahodha wa timu za taifa, makocha, mashabiki na wanahabari wataanza kupiga kura za kuchagua mchezaji bora hadi Agosti 10.

Baada ya hapo Fifa itatangaza wachezaji watatu wa mwisho ambao kati yao ndipo atatangazwa msindi mmoja katika hafla itakayofanyika London hapo Septemba 24.
 
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amejumuishwa miongoni mwa makocha 11, waliotajwa kuwania tuzo ya Kocha bora wa mwaka Fifa kwa wanaume.
Klopp amepewa nafasi hiyo ya kuwania tuzo hiyo kutokana na mafanikio aliyoyapata Liverpool, ikiwemo kuiwezesha kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, 2017-18.
Makocha wengine anaochuana nao ni pamoja na Kocha Massimiliano Allegri (Juventus), Stanislav Cherchesov (Russia), Zlatko Dalic (Croatia), Didier Deschamps (Ufaransa), Pep Guardiola (Manchester City), Roberto Martinez (Ubelgiji), Diego Simeone (Atletico Madrid), Gareth Southgate (England), Ernesto Valverde (Barcelona) na Zinedine Zidane (Real Madrid).
Kocha bora atatangazwa katika hafla itakayofanyika jijini London, Uingereza Septemba 24 mwaka huu, tuzo ambayo hupigiwa kura na makocha wa timu za Taifa, manahodha pamoja na waandishi wa habari.
 
Timu ya Inter Milan imegeuzia rada zake nchini Hispania ikitaka kufanya usajili wa kutisha kwa mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi katika dirisha la usajili msimu huu wa kiangazi.
Inter Milan imeingia kwenye rada ya usajili wa nyota huyo wa Barcelona na Argentina, ikiwa ni siku chache kupita tangu Juventus ilipomsajili na kumtangaza nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
 
Timu ya Inter Milan imegeuzia rada zake nchini Hispania ikitaka kufanya usajili wa kutisha kwa mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi katika dirisha la usajili msimu huu wa kiangazi.
Inter Milan imeingia kwenye rada ya usajili wa nyota huyo wa Barcelona na Argentina, ikiwa ni siku chache kupita tangu Juventus ilipomsajili na kumtangaza nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
 
Timu hiyo ya Italia inaelezwa imedhamiria kufanya usajili huo utakaotikisa dunia, wakimuwinda Messi kwa dau lolote ambalo wakala wake ataweka mezani.
Mashabiki wa Inter Milan tayari wameandika kwenye mitandao ya kijamii wakisema wanasubiri kwa hamu uongozi wa klabu yao wamsajili nyota huyo.
 
Back
Top Bottom