Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IYO feat. Harmonize

Nakupend


IYO Uhuh uhuh ai ololo lololo lolo ai Nakupenda eeh nakupendaa ooh I surrender my heart to you eh eh If you wanna be my lover I put my trust in you eh eh I can see no other (I can see no other) All i see is you (all I see is you) So me I want no other (me I want no other)

All I want is you ooh

Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh HARMONIZE na Rafael Lameck(kaandika) I treat you like a queen ubavu wa kushoto wa kulia Nyonga mkali ya hii na mambo ya kitoto siwezi rudia I no go liee mi kwa kukibu ndo siwezi ata kuhema Usinilagai ukawapa vidudu cha kusema Tukipata tutalala (ooh aba) tukikosa mashala (ooh aba)

Ata nguna kwa sangala (ooh aba) za osiku na sisindala (ooh aba)

Oh mapenzi penzi mchezo wa kitoto ogopa wache ucheze Mi nawe kama kurwa na doto peke yangu siwezi I'll die for you IYO I surrender my heart to you eh eh If you wanna my lover I put my trust in you eh eh I can see no other (I can see no other) All i see is you (all I see is you) So me I want no other (me I want no other) All I want is you eh eh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Oh my baby boo you're more than gold My love for you no go depreciate itappreciate We no go separate ooh eh What can I say there's nothing to say There's no word that is appropriate I de gyrate ooh because of you ooh Umenifunza mapenzi (nana) umenifunza kupenda (nana) Bila wewe siwezi (nana) usije niacha ukaenda (nana) Baby you give me love (nana) baby you give me happiness (nana) Baby you make me feel so good (nana) That's why I want to be with you ooh I surrender my heart to you eh eh If you wanna be my lover I put my trust in you eh eh I can see no other (I can see no other) All i see is you (all I see is you) So me I want no other (me I want no other) All I want is you ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Nakupenda aah ooh ooh so much I can offer ooh ooh Eh I love you baby eh I love you baby baby I need you baby ooh I need you baby baby more eh I love you baby ooh I need you baby baby oh I love yo baby eh I need you baby ooh It's yo Girl Iyo & Harmonize

[emoji634] Made with love & passion in Italy. [emoji289] Enjoyed everywhere
 
Tukio la askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Iramba mkoani Singida wanaodaiwa kusababisha ajali na kisha kutimua mbio limechukua sura mpya baada ya mabosi wao kuanzisha uchunguzi.

Kinachochunguzwa katika tukio hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu wawili, ni kujua chanzo cha askari hao kukimbia baada ya ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Kizanga.
 
Kamanda wa kikosi hicho nchini, Fortunatus Muslimu alisema jana kuwa uchunguzi utalenga kujua ni kwa nini askari hao walikimbia wakati walipaswa kutoa huduma kwa majeruhi pamoja na marehemu.

“Tunatuma maofisa wetu kwenda Singida kufanya uchunguzi tuweze kujua ni kwa nini baada ya tukio askari wetu walikimbia wakati walipaswa kutoa huduma. Lakini kingine kwa nini wananchi waliamua kuwafukuza askari eneo hilo,” alisema.
 
Katika tukio hilo, ndugu wawili wa familia moja walifariki dunia katika ajali hiyo iliyohusisha magari matatu katika kituo cha ukaguzi cha askari wa usalama barabarani kilichopo katika kijiji hicho.

Ajali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ndugu hao pamoja na wengine wakisafiri kwa gari aina ya Toyota Hiace kwenda Shelui kwa ajili ya kumjulia hali baba yao.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na askari hao kusimamisha magari bila utaratibu maalumu. Askari hao pia walipoteza mashine ya kutoa risiti za kielektroniki na tochi inayotumika kubaini mwendokasi wa magari.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba alisema tochi ilipatikana baadaye, lakini askari wake walitimua mbio wakihofia usalama wao.

Alisema ajali hiyo ilihusisha Hiace, lori mali ya kampuni ya Mtama ya mjini Bujumbura nchini Burudi na la kampuni ya Bakhresa.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Muslimu alisema katika suala hilo kuna mambo ya muhimu yanayopaswa kufahamika, hivyo watachukua hatua baada ya kufanya uchunguzi iwapo askari wanaolalamikiwa watabainika kuhusika.
 
Udhibiti wa ajali

Kuhusu ajali za barabarani, alisema wamefanya ukaguzi wa vyombo vya barabarani kati ya Julai 4 hadi 15 kwenye mikoa mbalimbali na kubaini kuwa kati ya madereva 878, madereva 225 hawakuwa na vyeti na 173 wamewafikisha mahakamani.

“Tutaendelea kufanya ukaguzi wa leseni ambapo wote tutakaowabaini hawana vyeti tutawanyang’anya leseni na kuwalazimu kwenda shuleni hadi watakapopata vyeti ndio waruhusiwe kuendelea” alisema Kamanda Muslimu.
 
Akizungumzia namna wanavyopambana na ajali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Juni Mosi hadi 30, wamekusanya Sh2.1 bilioni zilizotokana na tozo za makosa ya barabarani.
 
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), imesema chanzo cha kuwapima virusi vya Ukimwi watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 14 ni baada ya utafiti kuonyesha kundi hilo linaanza kujamiiana likiwa kuanzia miaka 10 na kuendelea.

Akitoa ripoti ya utafiti wa kitaifa wa viashiria na matokeo ya Ukimwi kwa mwaka 2016/17, mratibu wa Tacaids mkoa wa Tanga, Juma Billingi alisema utafiti huo kwa mara ya kwanza umewashirikisha watoto wadogo kwa sababu hizo.
 
Utafiti wa sasa umehusisha kwa mara ya kwanza watoto kuanzia miaka 0 mpaka 14; 14 hadi 49; na 50 na kuendelea,” alisema Billingi.

Pia, utafiti huu ulibaini wanandoa waliotalikiana wanaongoza kwa maambukizi kwa asilimia 11 na waliopo ndani ya ndoa ni asilimia 4.8

Akizungumzia watoto kuanza kujamiina wakiwa na umri mdogo, ofisa utafiti wa Tacaids, Dk Arodia Mulokozi alisema: “Wanafunzi wengi ni wanafunzi mchana tu usiku balaa tupu.”
 
Dk Mulokozi alisema baadhi ya wanafunzi wa avyuo vikuu ndiyo wapo hatarini zaidi hasa wanapofika mwaka wa pili.

“Hatari zaidi wakiingia mwaka wa kwanza wapolee wakifika wa pili siyo wale tena. Wengi wanapata ujauzito ina maana hawatumii kondomu,” alisema.

Awali, akizungumzia hali ya maambukizi, Billingi alisema: “Watanzania 81,000 wanapata maambukizi mapya kila mwaka sawa na asilimia 9.2.”
 
Pia, alisema mkoa unaoongoza kwa maambukizi ni Njombe wenye asilimia 11.4 ukifuatiwa na Iringa (11.3) huku mkoa wa mwisho wenye kiwango kidogo ukiwa ni Lindi (0.3).

Kuhusu kitafa, Billingi alisema kwa sasa kiwango cha maambukizi nchini ni asilimia 4.7 ukilinganisha na asilimia 5.1 miaka minne iliyopita.

Kitaifa, Billingi alisema kwa sasa kiwango cha maambukizi nchini ni asilimia 4.7 ikilinganisha na asilimia 5.1 miaka minne iliyopita.
 
Back
Top Bottom