Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alisema huo ni utafiti wa tatu kufanywa na Tacaids ambao unafanywa kila baada ya miaka minne.

Alisema wa kwanza ulifanyika 2007/08 na kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 7.5.

“Wa pili ulifanywa 2011/12 na matokeo yalionyesha kiwango kilikuwa 5.1 na sasa 2016/17 ndiyo hiyo asilimia 4.7,” alisema.

Alisema takwimu hizo ni himilivu kwa sababu hazipungui wala kuongezeka na kiwango cha maambukizi si kikubwa.
 
Mratibu huyo alisema kiwango cha maambukizi kwa wanawake ni asilimia 6.2 ukilinganisha na wanaume ambayo ni asilimia 3.1.

“Hawa ni wa miaka 15 mpaka 49,” alisema Billingi.

Alisema takwimu zinaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi kwa wanawake wanaoishi mjini ni asilimia 7.8 wakati wanaume ni asilimia 2.8.

Alisema makundi yaliyo hatarini zaidi kupata VVU ni wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, wanaofanya biashara ya ngono na watu wa mipakani.
 
Baada ya chumba kimoja cha biashara kati ya viwili vilivyokodishwa eneo la Sinza Afrikana kufungwa kwa muda kwa kutumia pingu, Jeshi la Polisi limesema kitendo hicho hakikuwa sahihi.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Salum Hamduni amesema pingu hizo zilifungwa eneo lisilo sahihi na hairuhusiwi kisheria.

Pingu hizo zilifungwa baada ya mpangaji aliyejulikana kwa jina la Glory Masawe anayeelezwa kuwa ni askari polisi wa kituo cha Oysterbay kuingia katika mzozo na Jerome Kaale mmiliki wa vyumba hivyo vya biashara.
 
Akizungumza na Mwananchi, Kamanda Hamduni alisema pingu zimetengenezwa kwa matumizi maalumu na zinatakiwa kutumiwa kwa utaratibu uliowekwa.

“Pingu ni kwa ajili ya kudhibiti wahalifu sugu na ambao wanaweza kutoroka wakiwa chini ya uangalizi. Kwa hiyo kufungwa eneo hilo si sahihi,” alisema.
 
Alisema wanaotakiwa kutumia pingu kisheria ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na wengine ambao sheria inawaruhusu.

Licha ya Masawe kukana kufunga pingu katika moja la milango ya maduka aliyopanga, mwenyekiti wa soko la Sinza II Afrikana, Ashrafu Msigiti alidai jana kuwa mpangaji huyo ndiye aliyefanya kitendo hicho ili kuhakikisha usalama wa mali zake.

Glory alipoulizwa na Mwananchi kuhusu kauli ya Msigiti alisema: “Si kweli bwana mimi sijui. Mimi naendelea kusema kuwa sikuwahi kufunga hizo pingu. Mimi nilivyokwenda kutoa vitu sijakuta pingu.”
 
Lakini, Msigiti alisema pingu hizo zilifungwa muda mrefu baada ya halmashauri kuzuia kufanyika biashara katika eneo hilo.

Alisema askari huyo alizuiwa kufanya biashara tangu Desemba mwaka jana baada ya halmashauri kutoa agizo kuwa eneo hilo halifai hasa biashara ya pombe. Alisema alitakiwa aondoke Julai 10.

“Baada ya hapo alikuja kuweka hizo pingu kwa madai kuwa anaongeza usalama ili vitu vyake visiibwe,” alisema Msigiti.
 
Hajafunga mtu mwingine ni yeye na alizitoa baada ya kuja kuchukua vitu vyake pamoja na hiyo milango.

Mmiliki wa vibanda hivyo, Kaale alisema mzozo ulianza baada ya Glory kudai arejeshewe fedha kutokana na kutaarifiwa na Manispaa ya Kinondoni kuwa eneo hilo halipaswi kutumika kwa biashara.

Alisema Julai 9, Glory aling’oa milango, madirisha na mita ya umeme katika hali anayoieleza ni ya kufidia fedha zake Sh1.8 milioni za pango.
 
Kaale alisema jana kuwa hajaridhishwa na uamuzi wa msaidizi wa mkuu wa kituo cha polisi cha Mabatini, Rijuo Said kuwa suala hilo lijadiliwe na uongozi wa serikali ya mitaa, hivyo atakwenda mahakamani kudai haki yake.

“Sitaishia hapa nitaenda mahakamani kwa kuwa nina haki ya kudai mali zangu ambazo zimechukuliwa bila ridhaa wala makubaliano,” alisema.

Alisema sasa anaandaa utaratibu wa kupata wakili ili kufungua kesi.
 
Mtuhumiwa ndo kwanza kaachia tabasamu.
20180725_131830.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nataka niwe kama malaika.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] shetani anakuona[emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom