Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji736][emoji736][emoji736][emoji736][emoji736][emoji736][emoji736]
130656cb-1bdd-442b-94d9-bcc1fd036db5.jpg
 
Kula Mlo kamili

Chagua kitu halisi, kamili, chenye lishe nzuri, cha mimea na chagua nyama ilio bora kama kuku wa kienyeji. vyakula ambavyo bibi na babu walikuwa wakivitumia. Achana na vyakaula vya kisasa, vya kwenye makopo. tengeneza chakula chako kiwe na rangi nzuri ya mimea, protein ya kawaida, na mafuta mazuri, vyakula vya kupaki vyenye sukari achana navyo.
 
Mbinu nzuri ni kula vyakula vingi vya mizizi na kufanya mazoezi ili mwili utoke jasho. Ondoa sumu kwa kula mbogamboga na matunda, hasa wakati wa asubuhi unaweza kula kabichi ya kutosha, au broccoli kwa ajili ya lunch, na ukala wali kidogo jioni na mboga za kutosha. tumia vyakula jamii ya kunde mara kwa mara.
 
Punguza sumu Kwenye mazingira yako.

Hewa chafu, madawa ya kuulia wadudu, mercury inayopatikana kwenye vipodozi na sehemu zingine . hivi vinasababisha sana saratani ya kibofu cha mkojo na saratani ya matiti , mirija ya uzazi. huwezi kuepuka vyote lakini unaweza kupunguza baadhi ya chemicals kwa kufanya uchunguzi wako mwenyewe.
 
Jali mwili wako, hasa utumbo wako.

Ndani ya tumbo lako kunahitaji afya ya hali ya juu. unaweza kutafuta mbinu za kusafisha sumu ilipo ndani yako. Tumia Dawa za antibiotics panapokuwa na umuhimu huo tu. Tena tumia zenye sifa na kuongeza kula chakula unapokuwa unatumia ili kusaidia kazi ya dawa hizo.

Vyakula vizuri vya kutumia mara kwa mara ni kama viazi vitamu, karanga, na mbegu za maboga. Mizizi inasaidia kuweka tumbo lako vizuri. utumbo unakuwa na afya nzuri .
 
Achana na Stress

Mtu mwenye stress anakuwa yupo kwenye hatari ya magonjwa mengi. Kumbuka kuwa stress inatokana na mambo mengi. Mahusiano mabaya, maisha sio mazuri, mawazo mabaya, kazi ambayo huipendi, yote haya yanaweza kusababisha saratani au ugonjwa wa akili. lakini ipo mbinu ya kuondoa au kupunguza . Nayo ni Meditation na mazoezi. tafuta mbinu ambazo zinafanya kazi kwa ajili yako na ufanye mara kwa mara.
 
Mazoezi ya kutembea kwa muda wa dakika 45 ni mazuri. fanya mazoezi kila siku au kila baada ya siku moja ili kujiepusha na saratani. wakati huo huo zingatia kutumia vyakula kama dawa. kwa kufanya hivyo utajiboresha katika kila vipengele vya afya ya mwili wako.
 
Back
Top Bottom