•Klabu ya UD Levante ya ya ligi kuu Hispania, imejitosa kuisaka saini ya mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta kutoka RC Genk kwa gharama ya euro 4milioni (€4m) (Sh 10.6bilioni).
…
•Levante imekuwa na mawasiliano na Samatta na sasa wanachosubiri ni kufikia makubaliano ya masuala yake binafsi huku gharama ya usajili wake ikikadiliwa kuwa euro 4milioni.
.
•Mshambuliaji huyo mwenye miaka 25, alisajiliwa na Genk mwezi Januari 2016 akitokea TP Mazembe kwa gharama euro 800,000.
.
•Samatta amecheza jumla ya mechi 53, za Ligi Kuu Ubelgiji pamoja na michezo 12 ya mashindano ya Europa Ligi. Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Samatta kutokana na kusumbuliwa na goti jambo lililomfanya acheze mechi 35.
.
•Samatta leo ataiongoza Genk katika mchezo wao wa kwanza wa kusaka kufuzu kwa mashindano ya Europa League dhidi ya Fola Esch ya Luxembourg.