Hii ni nafasi kwa Watanzania kuwatazama wachezaji wapya waliosajilia kwenye timu wanazozishabikia Ulaya, huu ni muda wa kutesti mitambo kwa timu mbalimbali Ulaya baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia," alisema Malisa.
Miongoni mwa vigogo wa soka la Ulaya wanaoshiriki katika mashindano hayo ni Bayern Munich, Borussia Dortmund za Ujerumani, Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal na Chelsea za England.
Nyingine ni PSG ya Ufaransa, Barcelona na Real za Hispania, AC Milan, Inter Milan na Juventus za Italia.