Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Cristiano Ronaldo

Kwa upande wa Ronaldo, soka ndiyo ilikuwa shule yake na mechi kubwa ndiyo ilikuwa mitihani yake. Akiwa mtoto mdogo, Ronaldo alicheza soka la ridhaa kwenye timu ya Andorinha kuanzia 1992 hadi 1995.

Baba yake alikuwa mtunza vifaa wa timu hiyo na miaka miwili baadaye akaenda kuichezea Nacional. Mwaka 1997, akiwa na umri wa miaka 12, alikwenda kufanya majaribio kwa siku tatu kwenye klabu ya Sporting CP, ambayo ilimsainisha kwa ada ya Pauni 1,500. Alijaribu kuwa mwanafunzi wa shule, lakini alifukuzwa baada ya kumrushia kiti mwalimu.
 
IMG-20180410-WA0000.jpg
 
Lionel Messi

Messi alijiunga na Rosario wakati akiwa na umri wa miaka sita. Kwa miaka hiyo sita aliichezea Newell’s, alionyesha kiwango bora kabisa na kutengeneza kumbukumbu ya kipekee kwenye timu hiyo. Baada ya mwaka mmoja kwenye akademia ya Barc elona, La Masia, Messi akaoro dheshwa kwenye Shirikisho la soka la Hispania (RFEF) Februari, 2002.
 
Baada ya kuka milisha tiba yake ya kutibiwa homoni za kumfanya akue kipindi akiwa na umri wa miaka 14, Messi aka weka rasmi kwenye kikosi cha timu ya Ba rcelona huko La Masia na sasa kuwa mchezaji mashuhuri kwenye kikosi hicho chenye maskani yake Nou Camp.
 
Neymar

Neymar alichanganya mapenzi yake ya futsal na soka la mitaani. Mwaka 2003, Neymar alihamia na familia yake Sao Vicente, ambako alikwenda kuichezea timu ya watoto ya Portuguesa Santista. Mwaka huohuo, alihamia Santos, ambako Neymar alikwenda kujiunga na Santos FC.
 
Kutokana na mafanikio yake, akisaidia kipato cha nyumbani na familia yake kuanza kununua nyumba jirani na Vila Belmiro. Familia yake ikawa vizuri baada ya Neymar kufikisha umri wa miaka 15, alikuwa akilipwa pesa nyingi. Akiwa na umri wake 17, alisaini mkataba wa kwanza kuchezea kikosi cha kwanza cha Santos na hapo akaanza kusaini dili tamutamu za kibiashara na sasa ni bonge la tajiri.
 
HALI bado inaonekana kuwa tete baina ya Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho na staa wake, Paul Pogba, ambaye ndio kwanza ametoka kutwaa Kombe la Dunia na kikosi cha Ufaransa kule Russia.

Na kama vile haitoshi, staa wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes, naye ni kama vile amerudia ukali wake wa zamani kwa nyota huyo akisema ‘inabidi atumie ubongo’ kuweza kuwa mwanasoka bora wa dunia.
 
Aliyeanza kuponda ni Mourinho aliposema kiwango ambacho Pogba ameonyesha katika Kombe la Dunia kinatokana na mpangilio wa mechi za michuano hiyo kuwa mfululizo tofauti na za Ligi Kuu England na michuano mengine.

“Sidhani kama ni suala la sisi kujaribu kumfanya awe bora, ni suala la yeye kutoa ubora alionao kwa ajili ya timu. Nadhani Kombe la Dunia ni sahihi kwa mchezaji kama yeye kuonyesha ubora,” alisema Mourinho.
 
Kwa nini? Kwa sababu ni michuano ya mfululizo mwezi mzima, ambapo mchezaji anaweza kuwaza soka tu. Anakuwa yupo kambini na wachezaji wenzake na anakuwa ametengwa na dunia ya nje. Kambi ni mechi tu ndizo ambazo zinakuhamasisha.

“Wakati wa msimu unaweza kuwa na mechi kubwa na mechi ndogo, halafu katika hizi hizi ndogo unaweza kupoteza uzingativu na unapoteza umakini. Halafu inakuja mechi kubwa.
 
Katika Kombe la Dunia hisia pamoja na majukumu siku zote zinakwenda juu. Unakuwa katika makundi, halafu unakwenda katika hatua ya 16, katika robo fainali, nusu fainali, kisha fainali. Hii inaleta hamasa na uzingativu kwa mchezaji. Nadhani Kombe la Dunia ni mazingira sahihi kwake.”

Kauli hiyo imekuja huku uhusiano wa Mourinho na Pogba ukitajwa kutokuwa mzuri hasa katika msimu uliopita ambapo kocha huyo aliwahi kumtoa Pogba katika mechi muhimu huku akimpiga benchi kwenye ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sevilla.
 
Naye Scholes, ambaye anajulikana kwa kutopendezwa na tabia za Pogba ndani na nje ya uwanja, amedai staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa anahitajika kuwa na mwendelezo wa ubora na asipotee uwanjani katika baadhi ya mechi kama ilivyo sasa.

“Pogba anahitaji kuwa na mwendelezo wa ubora nadhani. Unatazama jinsi anavyocheza, wiki hii anaweza kuwa bora sana, wiki ijayo asiwe mzuri. Anaonekana kuwa mchezaji ambaye anayeweza kucheza vizuri mara moja baada ya mechi nne. Kama mnataka kuchukua ubingwa wa ligi hali hiyo haitoshi,” alisema Scholes.

“Anahitajika kuwa mchezaji anayeweza kuamuru mechi kama ilivyokuwa Juventus. Alikuwa sehemu ya mfumo wa Juventus. Alijua kila wiki nafasi ambayo atakwenda kucheza na alijua atacheza na nani,” alisema.
 
Sidhani kama anasaidiwa hilo Manchester United kwa sababu itashangaza kama timu moja inaweza kutajwa mara mbili mfululizo katika fomesheni moja. Haijulikani atacheza vipi mechi ijayo na hilo halimsaidii.”

Pogba alipewa sifa nyingi katika Kombe la Dunia huku Ufaransa ikiichapa Croatia katika pambano la fainali na kushinda mabao 4-2 yeye akifunga moja katika pambano hilo lililochezwa Uwanja wa Luzhniki jijini Moscow.

Alisifika kwa kucheza vema katika eneo la kiungo hasa katika ushambuliaji na kutawanya mipira akilindwa vema kwa nyuma na kiungo mahiri wa Chelsea, N’Golo Kante pamoja na staa wa Juventus, Blaise Matuidi.

Maneno haya ya Mourinho na Scholes yanakuja wakati mashabiki wa Manchester United wakitaka kuona kiwango kitakachoonyeshwa na Pogba katika Ligi Kuu England msimu ujao.
 
Back
Top Bottom