Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], jamaniiii
 
Kocha Luiz Felipe Scolari, ameteuliwa kwa mara ya tatu kuinoa Klabu ya Palmeiras ya kwao Brazil.

Scolari mwenye miaka 69, amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo yenye maskani yake jijini Sao Paulo, timu iliyobeba ubingwa wa Brazil mara tisa.

Mara ya kwanza kwa Scolari kuimoa timu hiyo ilikuwa kati yam waka 1997 ma 2000, kabla ya kurejea mwaka 2010 siku chache baada ya kutimuliwa na Chelsea.
 
Kocha huyu aliipa Brazil ubingwa wa Dunia katika fainali zilizofanyika mwaka 2002 na akaiongoza tena Brazil katika fainali ya mwaka 2014, lakini hakuweza kuipa ubingwa badala yake akakutana na kipigo cha kihistoria cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani katika mchjezo wa nusu fainali.

Mara ya mwisho katika kazi ya ukocha Scolari alikua akiinoa klabu ya Guangzhou Evergrande ya China lakini akaiacha Novemba 2017, tangu wakati huo hawaja na timu ya kuinoa.
 
MASHABIKI wa Cristiano Ronaldo wanaomsubiri kwa hamu kubwa kumjuona nyota huyo akiliamsha ndani ya chama lake jipya la Juventus, wana kila sababu ya kutabasamu baada ya Star Times kuwapa mchomo mtamu.
Ipo hivi. kampuni hiyo imekuja na mashindano maalum ya kimataifa ya ICC ambayo yatatumika kumuonyesha mapema Ronaldo akiliamsha ndani ya klabu hiyo.
Ronaldo amejiunga na Juventus kipindi hiki cha usajili akitokea Real Madrid anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kitashiriki michuano ya ICC.
 
ICC ni michuano mahususi kwa timu kubwa za Ulaya kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa 2018/19. Michuano hiyo inahusisha timu 18 na Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa alisema Watanzania watapata nafasi ya kuwaona nyota wapya kwa timu zao katika mashindano hayo kupitia ving’amuzi vyao.
 
Hii ni nafasi kwa Watanzania kuwatazama wachezaji wapya waliosajilia kwenye timu wanazozishabikia Ulaya, huu ni muda wa kutesti mitambo kwa timu mbalimbali Ulaya baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia," alisema Malisa.
Miongoni mwa vigogo wa soka la Ulaya wanaoshiriki katika mashindano hayo ni Bayern Munich, Borussia Dortmund za Ujerumani, Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal na Chelsea za England.
Nyingine ni PSG ya Ufaransa, Barcelona na Real za Hispania, AC Milan, Inter Milan na Juventus za Italia.
 
Hata hivyo, kufikia ndoto za kucheza fainali za Kombe la Dunia hazihitaji kwenda shule, kwani kuna mastaa mahiri hao duniani, hawajawahi kwenda shule, lakini wamefanikiwa kucheza kwenye fainali za Kombe la Dunia, baadhi yao zikiwamo fainali za mwaka huu zilizomalizika wikiendi iliyopita huko Russia kwa mechi ya fainali kati ya Ufaransa na Croatia, huku Ufaransa wakiibuka mabingwa.
 
5. Ronaldinho

Ronaldo de Assis Moreira, maarufu zaidi kwa jina la Ronaldinho, alichagua soka mbele ya shule.

Kipaji chake cha soka kilianza kuonekana akiwa na umri wa miaka minane tu na hapo ndipo alipopachikwa jina la “Ronaldinho” kwa sababu alikuwa mchezaji mdogo zaidi katika mechi za timu za watoto.

Aliendelea kucheza kwenye futsal na soka la ufukweni na baadaye akaweka mkazo kwenye soka ambalo lilimfanya kuwa maarufu zaidi duniani.

Alikuwa gumzo akiwa na umri wa miaka 13 na kwenye mechi moja ambayo timu yake ilishinda 23-0, mabao yote siku hiyo alifunga yeye.
 
4. Didier Drogba

Drogba alizaliwa Abidjan, Ivory Coast na akiwa na umri wa miaka mitano alihamia Ufaransa na wazazi wake kwenda kuishi kwa mjomba wake, Michel Goba, aliyekuwa mwanasoka. Lakini ghafla

Drogba akakumbuka nyumbani, hivyo akarudi Abidjan baada ya miaka mitatu tu. Lakini, wazazi wake wote wawili wakapoteza kazi zao, hivyo Drogba ilibidi arudi tena kwa mjomba wake.

Hakupata nafasi ya kwenda shule, hivyo akajiunga moja kwa moja kwenye klabu ya Levallois
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…