Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JELA? Ndio. Staa mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo amehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika mamlaka za Hispania, lakini bahati nzuri kwake ni hatakwenda jela.

Ronaldo alikiri kosa hilo la kukwepa kodi na kukubali hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela pamoja na faini ya Pauni 16.9 milioni, lakini hatakwenda jela kwa sababu sheria za nchi hiyo zinazuia mtu aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kosa hilo kwenda jela.
 
Staa huyo wa kimataifa wa Ureno, alikuwa akitafuta suluhu baada ya kupatikana na hatia ya makosa manne ya ukwepaji wa kodi kati ya mwaka 2011 na 2014. Jumla ya kiasi alichokwenda kilikadiriwa kufikia Pauni 13 milioni.

Hata hivyo, kiasi hicho cha kodi kilipunguzwa kwa Pauni 5 milioni kama sehemu ya makubaliano, lakini gharama nyingine pamoja na faini zilimlazimisha Ronaldo kutoa Pauni 16 milioni ili kumaliza shauri lenyewe.
 
Inadaiwa makubaliano kati ya wawakilishi wa Ronaldo na watu wa serikali yalifikiwa kwa muda mrefu, lakini walilazimika kusubiri Serikali mpya ya nchi hiyo kuafiki masharti mbalimbali ya suala hillo la muda mrefu.

Ronaldo alitaka kumalizana vyema na mamlaka za nchi hiyo kwa ajili ya kujikita zaidi katika soka baada ya kutua Juventus kwa dau la Pauni 88 milioni akitokea Real Madrid mapema mwezi huu katika uhamisho ulioshangaza mashabiki.
 
Kabla ya hapo alikuwa anapambana na mashtaka hayo, lakini ameamua kuafiki kila kitu kwa sababu anataka kuanza maisha mapya nchini Italia bila ya usumbufu baada ya kukipiga nchini Hispania kwa kipindi cha miaka tisa akitokea England.

Ronaldo anakuwa staa mwingine mkubwa aliyecheza Hispania kuingia katika migogoro ya kodi na mamlaka za nchi hiyo.
 
Mwaka jana hasimu wake mkubwa, Lionel Messi alihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela pamoja na baba yake kwa kosa la kukwepa kodi kiasi cha pauni 3.5 milioni.

Hata hivyo, kama ilivyo kwa Ronaldo, Messi na baba yake hawakwenda jela kwa sababu kifungo hicho hakikuzidi miaka miwili na staa huyo alimaliza kesi hiyo kwa kuamua kulipa mamlaka hiyo na hivyo, kuendelea kupeta katika maisha yake ya soka kama kawaida.
 
Aisee....
 
Staa mwingine, ambaye aliwahi kuonja makali ya mamlaka hizo ni nyota wa zamani wa Barcelona, Javier Mascherano aliyewahi kuhukumiwa mwaka mmoja na faini kwa kosa ya kukwepa kulipa kodi mwaka 2016.Hata hivyo, hakutimkia jela.

Mwingine ni staa wa zamani wa Barcelona, Alexis Sanchez ambaye kwa sasa anakipiga Manchester United.
 
Februari mwaka huu alihukumiwa kifungo cha miezi 16 jela na faini kwa kosa la kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2012 na mwaka 2013.

Kutokana na hukumu hiyo, staa huyo alishindwa kwenda Marekani na wenzake wa Manchester United katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya, baada ya ubalozi wa Marekani nchini England kumnyima visa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…