Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amepanga kuwatumia wachezaji chipukizi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea wikiendi hii.
Uamuzi huo umefikiwa na Kocha huyo baada ya yosa wake kuitandika Bayern Munich kwa mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa Jumamosi mjini Miami, Marekani.
Guardiola ambaye aliwapa wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza mapumziko baada ya kuzitumikia nchi zao katika fainali za Kombe la Dunia 2018, ameona kikosi hicho kinaweza kumpa mafanikio.
 
Ametamba kuwa haoni hatari kuwatumia yoso kama Phil Foden,18, Brahim Diaz,18 na Eric Garcia, 17, akiamini wao uwezo wa kuiduwaza Chelsea na kutwaa Ngao ya Jamii ukiwa ni mwanzo mzuri wa msimu mpya wa Ligi.
“Bado tumesaliwa na siku tano ama sita kabla ya kucheza mechi Ngao ya Jamii nadhani huu ni muda mfupi sana kujiandaa kwa wachezaji wanaotoka mapumzikoni kwa hiyo tumepanga kuwatumia vijana ambao wameonyesha dalili nzuri kwenye mechi za majaribio,” alisema.
 
UKALI wa Jose Mourinho haujawahi kumuacha mtu salama. Hata kama ni bosi wake. Baada ya kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa wapinzani wao Liverpool pambano la kirafiki juzi usiku wa manane, kocha huyo mreno amewabwatukia mabosi wake kwa kushindwa kununua mastaa wapya.

United ilipokea kichapo hicho jijini Michigan Marekani lakini mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo, Mourinho alipeleka ujumbe kwa matajiri wa United jinsi wanavyomkwaza kwa kushindwa kuwanunua wachezaji mahiri wapya.
 
Mpaka sasa amefanikiwa kumnasa kiungo wa kimataifa wa Brazil, Fred kutoka Shakhtar, kinda wa Ureno, Diogo Dalot kutoka Porto pamoja na kipa mkongwe, Lee Grant kutoka Stoke City kwa ajili ya kuwa mchezaji wa akiba zaidi.

Mourinho amedai anahitaji kununua wachezaji wawili kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Agosti 9 ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England. Hata hivyo, ana wasiwasi huenda akampata mchezaji mmoja tu.
 
Amedai kuna nafasi ambayo anataka mchezaji mmoja tu lakini aliwapa majina matano matajiri wake ingawa mpaka sasa wameshindwa kupata mtu katika nafasi hiyo na hivyo kumuacha akiwa anahaha.

“Nadhani sitawapata wachezaji hao wawili. Inawezekana labda nikampata mmoja na kuna nafasi moja niliipa klabu majina matano miezi michache iliyopita kwa hiyo nasubiri tu kama itawezekana,” alisema kwa unyonge Mourinho.
 
Tulianza mechi (dhidi ya Liverpool) na wachezaji wengi ambao hawatakuwepo katika kikosi Agosti 9. Hiki sio kikosi changu, hakifiki hata nusu, haifiki hata asilimia 30 ya kikosi changu,” aliongeza kocha huyo huku pia akilalamikia idadi ya mashabiki wachache wanaojitokeza viwanjani. Mourinho pia amelalamikia klabu zimekuwa zikipeleka vikosi hafifu Marekani katika mechi hizi za maandalizi, kitu ambacho anakiona kama utapeli wa pesa kwa mashabiki wa nchini humo ambao wangetamani kuwaona wachezaji mastaa.
 
Hali ya uwanja ilikuwa nzuri lakini kama ningekuwa wao nisingekuja uwanjani. Nisingepoteza pesa yangu kutazama hizi timu. nilitazama mechi ya Chelsea na Inter Milan kabla ya hapo na uwanja ulikuwa mtupu. Hawa watu walikuja hapa kwa sababu wanapenda timu zao.

“Mashabiki wa Marekani wanastahili zaidi ya hivi. Wanahiitaji United nzuri, Liverpool nzuri, Real Madrid nzuri. Nawaonea huruma jinsi wanavyofanya promosheni ya soka nchini hapa,” aliongeza kocha huyo wa zamani wa Chelsea.
 
Mastaa ambao wanakosekana katika kambi ya United kwa sasa ni wale ambao timu zao za taifa zilifika mbali katika Kombe la Dunia zilizomalika Russia hasa kwa timu ambazo zilitinga hatua ya nusu fainali ya fainali hizo.

Mastaa kama Romelu Lukaku, Marouane Fellaini, Paul Pogba, Ashley Young, Jesse Lingard na Marcus Rashford wameendelea kufanya matanuzi katika likizo zao baada ya kuongezewa siku za kupumzika kutokana na nchi zao kufika nusu fainali pale Russia.
 
Kambi ya United inaonekana kuvurugika zaidi baada ya staa, Anthony Martial kuondoka kwa ajili ya kushuhudia kuzaliwa kwa mtoto wake wa pili kule Ufaransa huku kiungo mahiri, Nemanja Matic akitazamiwa kuikosa mechi yake ya kwanza dhidi ya Leicester City baada ya kufanyiwa operesheni ambayo Mourinho hakutaka kuifafanua.

Inajulikana Mourinho anamfukuzia kwa karibu beki wa Leicester City na Timu ya Taifa ya England, Harry Maguire ili kuimarisha safu ya ulinzi.
 
Menstruation Testimony!*

During church service, this 16-year old pastor's daughter stood up and said: "Praise the Lord!" Everybody shouted with joy: "Hallelujah!!". She continued:
"Since the age of 13, I've been experiencing painful monthly periods. But now, after a series of Bible studies and prayers with brother Solomon in his house, my monthly periods have stopped for more than 3 months now. No more pain, no more menstruation. You can see I'm even getting fatter and prettier. We are starting to pray seriously about the small problem of vomiting, especially in the morning. Praise the Lord".
The whole church was silent... and
Brother Solomon fainted!!!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom