Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1533098724538.jpg
 
Nimeonja Pendo
(3_01 Agosti 2018)

MTAGUSO, FAHARI YA KANISA KATOLIKI

Leo tuanze safari ya kuutazama MTAGUSO ndani ya kanisa.

Kifupi, MTAGUSO ni kama vile mkutano mkuu wa kanisa katoliki, unaojadili na kuamua mambo makubwa yahusuyo namna ya kuliendesha kanisa na kulifanya liweze kweli kueneza ufalme wa Mungu hapa duniani huku likimsaidia mwanadamu kurudi kwa Mungu wake baada ya maisha ya hapa duniani.

Kwa kawaida na kwa karne za hivi karibuni, mtaguso huitishwa na Papa, na huhusisha maaskofu, wakuu wa mashirika ya Kitawa ya kiulimwengu, makardinali, na watu wengine kadhaa wanaoalikwa maalumu na Papa kwa sababu maalumu.

Kuna watu hudhani maaskofu wote duniani huhudhuria mtaguso, jambo ambalo sio kweli. Kwa mfano, kwa sasa inakadiriwa kanisa lina maaskofu takribani 2,500 ulimwenguni kote, hivyo sio rahisi kuwaita wote kwenye kikao kimoja na wote wakapata nafasi ya kuchangia. Badala yake huitwa kiuwakilishi kadiri ya nchi, kanda, rika, taaluma, uzoefu, ubobevu, karama, uhitajikaji au mahitaji maalumu, na vigezo vingine kama hivyo.

Miongoni mwa maamuzi makubwa yanayofanywa na Mtaguso ni pamoja na kuweka au kuboresha sheria za kanisa (canons), kanuni za kanisa, kanuni za kiibada/kiliturujia, misimamo ya kanisa, mafundisho ya kanisa, kanuni za kiutawala/kiuendeshaji, tafsiri za misingi ya imani kadiri ya maandiko matakatifu na mapokeo ya kanisa, nk.

Mara chache imetokea mtaguso ukawa mfupi kwa siku chache tu. Lakini mara kadhaa imetokea mtaguso ukawa mrefu, na hata wakati wingine umekuwa mrefu kiasi cha kuchukua miaka kadhaa kwamba wajumbe wakakaa vikao kadhaa kwa awamu, wakatawanyika na kurudi tena.., na hata pia wakati mwingine baadhi ya wajumbe wakabadilika (baadhi kutokurudi tena na baahi wapya kuingia) katika mtaguso huo huo mmoja kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhitaji, kufariki, kustaafu nk.

Tangu kuanza kwa kanisa katoliki ulimwenguni (mwaka 33 BK), kumekuwepo na jumla ya Mitaguso 22 au 21. Kiuhalisia kabisa mitaguso ni 22, ingawa wengi huuondoa mtaguso wa kwanza kabisa kuwepo, wa mwaka 50 BK kwa sababu ya namna ambavyo mtaguso huo uliitishwa na kuendeshwa. Ulikuwa wa kidemokrasia kwa asilimia nyingi sana kuliko kuwa wa kichungaji, jambo lililoufanya ufanane zaidi na mkutano wa wanachama wa chama fulani badala ya mjadala wa kikanisa. Hata hivyo ni vigumu kuupuuza moja kwa moja kwa sababu ni mtaguso wenye mchango mkubwa ingawa ulibanwa na ile dhana inenwayo "mwanzo mgumu".

Mitaguso imegawanyika katika makundi matatu au manne hivi. Kwanza ni huo mtaguso wa awali ambao nimesema baadhi ya wataalamu wa mambo ya kanisa hawautambui. Pili ni mitaguso ya kipindi ukristo unaenea Ulaya nje ya Israeli. Tatu ni mitaguso ya kipindi cha uzushi kilichoshuhudia mamlaka ya Papa yakipingwa vikali na hasa yakijaribiwa kuwekwa chini ya maamuzi ya mtaguso, yaani kipindi sumu ya demokrasia ilipotaka kulitafuna kanisa. Na nne ni Mitaguso mikuu, mitaguso ya kipindi cha ukomavu wa kanisa.

Orodha ya mitaguso yote 22 (au 21) na miaka yake kwenye mabano ni hii:

1. Mtaguso wa Yerusalemu (50)

2. Mtaguso wa Nicaea - I (325)

3. Mtaguso wa Constantinopoli - I (381)

4. Mtaguso wa Efeso (431)

5. Mtaguso wa Chalcedon (451)

6. Mtaguso wa Constantinopoli - II (553)

7. Mtaguso wa Constantunopoli - III (680 - 681)

8. Mtaguso wa Nicaea - II (787)

9. Mtaguso wa Constantinopoli -IV ( 869 - 870)

10. Mtaguso wa Laterano - I (1123)

11. Laterano - II (1139)

12. Laterano - III ( 1179)

13. Laterano - IV ( 1215)

14. Mtaguso wa Lyon - I (1245)

15. Mtaguso wa Lyon -II (1274)

16. Mtaguso wa Viane (1311 - 1312)

17. Mtaguso mkuu wa Constance (1414 - 1418)

18. Mtaguso mkuu wa Basel, Ferrara, Florence na Roma (1431 - 1442)

19. Mtaguso mkuu wa Laterano - V (1512 - 1517)

20. Mtaguso mkuu wa Toronto (1551 - 1552 na 1559 - 1565)

21. Mtaguso mkuu wa Vatikano - I (1869 - 1870)

22. Mtaguso mkuu wa Vatikano - II (1962 - 1965).

Tukipana fursa wakati mwingine tutatazama kwa undani mtaguso mmoja baada ya mwingine. Ulifanyika kwa malengo gani, ulilizalia kanisa matunda gani, ulikuwa na matokeo gani au manufaa yake kwa kanisa mpaka leo ni yapi, changamoto zake ni zipi, kwa nini ulifanyika katika mji huo, kwanini baadhi ya mitaguso imejirudia kufanyika katika mji mmoja mara kadhaa, kwanini mitaguso imegawanyika katika makundi manne, nk.

Na hatimaye tutamaliza na mtaguso mkuu wa pili wa Vatikano ambao ndio wa mwisho mpaka sasa na wenye mchango mkubwa kwa kanisa la leo kuliko mitaguso mingine mingi. Huu, tukijaliwa tutachambua hati zake moja baada ya nyingine kuona zinaliongozaje kanisa la leo na sisi tunaziishije ili kujipatia wokovu utokao kwa Mungu wetu.

Karibuni kwa tafakari.

#nimeonjapendo
Binafsi sijaona dosari, maana nia yako ni kutujuza hivyo kwetu ni kujifunza. cha msingi utambue kuwa povu halina nafasi mahali hapa
 
Back
Top Bottom