Mpenzi wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo, kaamua kuhamia jumla na wanawe kutoka Madrid, Uhispania hadi mjini Turin, Italia ili kuwa karibu na mpenzi staa huyo.
Kulikuwa na tetesi kwamba baada ya CR7 kuhamia Italia baada ya kusajiliwa na Juventus, Georgina angebakia Uhipania kwenye makazi ya straika huyo au arudi nyumbani Ureno kwa ajili ya kuangalia familia.
Hata hivyo, ripoti zimeeleza kuwa Cristiano anataka kuwa karibu na watoto wake wote wane, hivyo Georgina atalazimika kuongozana nao na kuachana na shughuli zote alizokuwa akifanya Uhispania ili akawe mke nyumbani kule Italia.
Mrembo huyo alipata mtoto mmoja binti na straika huyo mwenye miaka 34. Hata hivyo Cristiano ana mtoto mwingine wa kiume Cristiano Jr aliyezaa na hawara mmoja na pia pacha aliolipa mwanamke mmoja wa kule Marekani baada ya kumbebea ujauzito.