Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

446625954_223929.jpg
 
Nyoka mmoja aliingia kwenye karakana ya seremala. Kulikuwa na msumeno umeanguka chini. Kwa bahati mbaya ulimgusa nyoka, akaumia kidogo. Kwa hasira, nyoka aliung'ata ule msumeno. Alipoung'ata ule msumeno, aliumia tena (kwa kuwa ni wa chuma). Alipoona anazidi kuumia, akaouna ule msumeno ni adui m'baya sana. Ikabidi atumie nguvu zaidi kuung'ata. Akaamua kujizungusha kwa nguvu kwenye msumeno ule ili aubane na kuunyongelea mbali kabisa. Masikini... Nyoka yule aliishia kujiua mwenyewe kwa hasira zake juu ya msumeno. - - FUNZO: Katika maisha, mara nyingine tunafanya maamuzi kwa hasira sana kwa lengo la kumuumiza yule aliyetukosea, bila kujua tunajiumiza wenyewe. Tujifunze kusamehe na kudharau baadhi ya watu, matukio, na vitu vilivyotukwaza iwapo kufanya hivyo hakutatuumiza zaidi.
@Numbisa. Nyoka wako huyu hapa amepatikana [emoji16][emoji16][emoji16]
IMG-20180801-WA0036.jpg
 
KAZI nzuri inalipa. Ndiyo hivyo, baada ya Chelsea kukubali mziki wa kiungo wake matata kabisa, mkata umeme, N'Golo Kante na hivyo kumwaandalia mkataba mpya wa miaka mitano na mshahara wa Pauni 290,000 kila wiki.
Habari ndiyo hiyo. Chelsea inafanya hivyo ili kuwakata kilimilimi wale wanaomfukuzia kiungo wake huyo, hasa Paris Saint-Germain, ambayo inaonekana udenda kuitoka ikiitaka huduma yake.
Mkataba wa sasa uliobaki huyo Stamford Bridge ni miaka miwili, lakini kwa dili hilo jipya ambalo litamfanya aweke kibindoni Pauni 75 milioni litakwenda kukomea mwaka 2023.
 
Mshahara huo mpya utamfanya Kante kulipwa pesa nyingi zaidi, zaidi ya Pauni 70,000 anazolipwa Eden Hazard, ambaye pia anaweza kusainishwa dili jipya ili kumfanya asishawishike kwenda Real Madrid.
Mabingwa wa Ufaransa PSG wamemweka Kante kwenye chaguo lao la kwanza la wachezaji inaowataka, lakini kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri anataka kubaki na wachezaji wake wote bora akiwamo Hazard na Willian katika msimu wake wa kwanza.
Lakini shida inayowakabili Chelsea ipo kwa kipa Thibaut Courtois, ambaye ameripotiwa kuwaambia wababe hao wa London wakubali tu kumuuza kwenye dirisha hili la sivyo ataondoka bure mwakani.
 
WANASEMA hivi, dawa ya jeuri kiburi. Winga Anthony Martial anawafanyia jeuri Manchester United, basi nao wameamua kumjibu baada ya kuelezwa watafyeka mshahara wiki mbili kutokana na kitendo chake cha kutoweka mazoezini kwa siku nane.
Imeelezwa hivi, kutokana na hilo, Martial ambaye aliondoka kambini kwenda kwa mpenzi wake, Melanie Da Cruz, aliyejifungua mtoto hivi karibuni, ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake kwa siku nane na hivyo, panga kali litapita kwenye mshahara wake, baada ya kumpiga faini ya Pauni 180,000 ambayo ni sawa na mshahara wake wa wiki mbili
 
Kwahiyo huyo aliyesema bikra inamaana mumewe hakuwahi hata mara moja?kabisaaa??

Naona na dada yao leo kaolewa na yule mchezaji wa south
Kale kajamaa kalikurupuka ili mradi tu na kenyewe kaonekane kideon harusin kwa kaka

Hope dada mtu katulia maana nimeona mahali wanauliza kama hio couple ilipima homa kubwa(maana bwana harusi alikua anatoka na jini kabula)
 
Back
Top Bottom