Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna jamaa mtaani ako na kashop na ni mjinga sana. Last night, I went to buy condoms, he told me zimeisha.
Leo morning, when my wife went to buy bread, he told her to tell me that the condoms I was looking for are now available. Sasa ile vita iko kwangu ni worse than Syria.[emoji879][emoji879]
 
KUPANGA ni kuchagua na Arsenal inaonekana ina jambo lake inalolipanga kulifanya kwenye dirisha hili la usajili.
Wababe hao wa Emirates si unajua Ligi Kuu England ikianza itakuwa chini ya kocha mpya, Unai Emery, hivyo jitihada kubwa zimewekwa kwenye kusajili wachezaji ambao wataifanya Arsenal kuwa timu tofauti na ilivyokuwa chini ya kocha wa zamani, Arsene Wenger.
 
15331429659141513764736.jpg
 
Mpango wa Emery ni kufanya usajili wa mastaa wa maana tupu na ndiyo maana kwa sasa mkakati uliopo ni kumpiga bei kiungo Aaron Ramsey ili zipatikane pesa zitakazotosha kumsajili staa wa Sevilla na Ufaransa, Steven N'Zonzi.
Ripoti zinadai Emery ameshatumia bajeti yake ya Pauni 70 milioni, hivyo amepungukiwa pesa ya kumpata Nzonzi, jambo ambalo Ramsey sasa itabidi atumike kupatikana kwa pesa ya kufanyia usajili.
 
Emery aliwahi kufanya kazi na N'Zonzi walipokuwa pamoja huko Sevilla, hivyo anaamini katika uwezo wake kwamba akitua kwenye kikosi cha Arsenal atakuwa na msaada mkubwa.
N'Zonzi ataigharimu Arsenal walau Pauni 25 milioni na inaamini kiasi hicho cha pesa inaweza kukipata kwenye mauzo ya Ramsey, ambaye bado anagoma kusaini mkataba mpya kwenye kikosi hicho cha Emirates.
Arsenal imempa Ramsey ofa ya mkataba wa miaka mitano, lakini hadi sasa bado hajausaini.
 
STAA wa zamani wa Arsenal na Ufaransa, Thierry Henry amewekwa kwenye orodha ya makocha ambao wanatarajia kupewa kibarua cha kuinoa Timu ya Taifa ya Misri, inayochezewa na supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah.
Chama cha Soka cha Misri kinamtaka Henry, aliyewahi kuichezea pia Barcelona, ambaye pia alikuwa kocha msaidizi wa Ubelgiji katika fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika huko Russia kwenda kuchukua mikoba ya Hector Cuper, aliyefutwa kazi baada ya Mafarao kupoteza mechi zote tatu za hatua ya makundi ilizocheza kwenye fainali hizo.
 
Wiki iliyopita, Henry alihusishwa pia kwenye mpango wa kuwa kocha wa Aston Villa kabla ya mabosi wa klabu hiyo ya Championship kuamua kubaki na Steve Bruce.
Wakala Nader El-Sayed alisema Henry anaonekana kuwa tayari kupokea kibarua hicho kitakachompa nafasi ya kumnoa mchezaji matata kabisa kwa sasa, Mo Salah.
 
Kinachoelezwa ni Misri wanasubiriwa kubainisha programu zao wanazotaka, lakini jambo kubwa ni Henry mwenyewe kujiweka kwenye mazingira ya kukubali kazi ya ukocha mkuu kwenye timu hiyo ya Afrika.
Henry mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa bado ni msaidizi wa Roberto Martinez kwenye kikosi cha Ubelgiji.
 
Back
Top Bottom