STAA wa zamani wa Arsenal na Ufaransa, Thierry Henry amewekwa kwenye orodha ya makocha ambao wanatarajia kupewa kibarua cha kuinoa Timu ya Taifa ya Misri, inayochezewa na supastaa wa Liverpool, Mohamed Salah.
Chama cha Soka cha Misri kinamtaka Henry, aliyewahi kuichezea pia Barcelona, ambaye pia alikuwa kocha msaidizi wa Ubelgiji katika fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika huko Russia kwenda kuchukua mikoba ya Hector Cuper, aliyefutwa kazi baada ya Mafarao kupoteza mechi zote tatu za hatua ya makundi ilizocheza kwenye fainali hizo.