Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jaman jaman,,,muoneni huyu binti[emoji23] [emoji23] [emoji23] ,,,,muongope Mungu wako,,, bora hata mm niseme enzi zetu hz bhana,, na zile suruali za pekosi[emoji124] [emoji124]
Waone ma andaeitini kupenda jivika uhenga[emoji23][emoji23][emoji23]nyie subirini muda wenu ufike zilipendwa zenu zitakuwa kwangwaru,sijui kibegi[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Enzi zetu hizo akina ya buyenze ,mzee fenesi hawafahamu utamu wa hizi dansi[emoji125][emoji125]
 
Kijana, umeiona hiyo tarehe kwenye tangazo?
Ni kipindi bendi nyingi za muziki zilikuwa bado zinaimba nyimbo za kuyasifu majeshi yetu baada ya vita kuisha, ccm ndio kwaaanza ina miaka minne tangu "kuzaliwa",nyimbo nyingi ilikuwa ni kusisitiza tufunge mikanda, tufanye kazi kwa bidii.
Kulikuwa hakuna mtu maarufu wa kutajwa tajwa kwenye nyimbo kama sasa zaidi ya Nyerere na kidogo Kawawa...
Miaka hiyo ndio kipindi pekee ambacho wanafunzi walikuwa hawakaguliwi viatu maana hata waalimu wengine walikuwa hawavai viatu.
Ndo kipindi pekee mama, baba, mjomba au shangazi akitoka Dar wanakijiji wote watafika kumsalimia na kumshangaa lafudhi yake ilivyo athiriwa na Kiswahili.

Habari ya majukumu kijana wangu[emoji23] [emoji23] [emoji137]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…