Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HUKO England kumenoga, ni amshaamsha tu. Ile mikikimikiki ya Ligi Kuu England imerudi rasmi, usiku wa jana Ijumaa kulikuwa na mechi moja, lakini uhondo kamili unaanza leo Jumamosi na kuendelea kesho Jumapili.

Jana Manchester United ilikuwa na shughuli pevu huko Old Trafford ilipoikaribisha Leicester City na hiyo ilikuwa mechi ya kufungua pazia la Ligi Kuu England, ambapo kila kocha anajaribu kusaka njia za kuubeba ubingwa ambao msimu uliopita ulinyakuliwa na Manchester City ya Pep Guardiola.
 
Utamu wa ligi hiyo kwa timu za Top Six kwa msimu huu ni kwamba kutakuwa na makocha wawili wageni, Unai Emery huko Arsenal na Maurizio Sarri huko Chelsea.

Makocha hao wanakuja kuwapa changamoto wenyeji wao, Guardiola wa Man City, Jose Mourinho wa Man United, Jurgen Klopp wa Liverpool na Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur.

Mchakamchaka wa msimu huu utashuhudia pia mastaa wa kigeni kibao wakitua kwenye Ligi Kuu England kuongeza uhondo utakaofanya utamu wa michuano hiyo pengine kuzidi misimu uliopita.
 
Mechi ya kwanza itakayofanyika mchana wa leo Jumamosi, Newcastle United inayonolewa na Rafa Benitez itakuwa nyumbani kuikaribisha Spurs, mechi inayotazamwa itakuwa ngumu kwelikweli kabla ya Bournemouth kumaliza ubishi na Cardiff City, Fulham ikiwa na mastaa wapya kibao wakishuka uwanjani kucheza na Crystal Palace, Watford ikicheza na Brighton na Wolves itakuwa na kasheshe mbele ya Everton. Kocha Sarri ataanzia shughuli ya Ligi Kuu England ugenini wakati atakapoifuata Huddersfield.
 
Lakini yote hiyo ni tisa, kumi bana ni vipute vya hiyo kesho Jumapili. Huko Emirates kutakuwa na kasheshe zito, wakati Emery na chama lake la Arsenal watakapowakaribisha mabingwa watetezi Man City.

Mechi hiyo inatarajia kuwa na ufundi mkubwa, huku Arsenal ikiingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa Tatu Bila katika mechi ya mwisho ya ligi ilipocheza uwanjani Emirates dhidi ya vijana hao wa Guardiola.

Lakini mechi hiyo ya baadaye, itatanguliwa na mechi mbili matata, wakati Liverpool itakapokuwa Anfield kuikaribisha West Ham United, ambayo imefanya usajili mkubwa sana kwenye dirisha lililofungwa juzi Alhamisi.
 
KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema amekuwa na matarajio makubwa ya kufanya kweli kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Kocha huyo wa wababe hao wa Anfield aliiwezesha Liverpool kumaliza ligi ya msimu uliopita kwenye nafasi ya nne, lakini baada ya kufanya usajili mkubwa anaamini safari hii ni zamu yao ya kufanya vizuri zaidi.

Mjerumani huyo ametumia zaidi ya Pauni 160 milioni kwenye dirisha la usajili na kuamini amewanyakua wachezaji ambao wataifanya timu yake kuwa moto zaidi ndani ya uwanja.
 
Wachezaji ambao Klopp amewanasa ni Naby Keita, Fabinho, Alisson Becker na Xherdan Shaqiri, ambapo ujio wao wakikutana na wakali wengine kama Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino wataifanya Liverpool kuwa timu ya kuipitia mbali.

Klopp alisema: "Matarajio yangu siku zote ni makubwa. Tutajaribu kufikia nafasi za juu zaidi.

"Ni jambo la kawaida kutumia pesa nyingi kuliko miaka mingine. Unapaswa kuandaa kikosi ambacho kitakuwa na wigo mpana na kuweza kupambana na mikikimikiki ya Ligi Kuu."
 
KAMA uliweka ulibeti kwa kuipa ushindi Leicester City kwenye mchezo wa kwanza wa kuchana pazia la Ligi Kuu ya England msimu huu, basi utakuwa umeuchana mkeka wako kiulaini kabisa mwanangu.

Ndio! Mashabiki wengi wakiwemo wa United wenyewe hawakuwa na uhakika kama timu yao inaweza kushinda kwenye mchezo huo kutokana na kushindwa kuvunja akaunti na kufanya usajili wa maana.

Lakini, kutofanya usajili hakujawahi kuwa tatizo kwa kocha Mreno, Jose Mourinho ambaye usiku huu (jana Ijumaa) ameiongoza timu yake kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester City kwenye dimba la Old Trafford.
 
Mabao mawili ya kiungo fundi wa Kifaransa, Paul Pogba na beki Luke Shaw yalitosha kumfanya Mourinho kupata usingizi mororo na kuanza kwa ushindi na kuliweka jeshi lake kileleni mwa msimamo.

Alianza Pogba aliyeiweka United mbele kwa bao 1-0 akifunga kwa mkwaju wa penalti kwenye dakika ya tatu tu ya mchezo.

Kiungo huyo ambaye aliomba kuuzwa kwenda Barcelona, lakini mabosi wa Man United wakaweka ngumu, alipachika mkwaju huo baada ya beki Daniel Amartey kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti.
 
Kuingia kwa bao hilo hakukuwafanya Leicester City kuwa wanyonge na badala yake waliliandama lango la United, lakini walishindwa kutumia nafasi kadhaa walizotengeneza kwenye kipindi cha kwanza.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Man United ilikuwa mbele kwa bao 1-0. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Man United ikionekana kucheza kwa tahadhari zaidi na kupoza mipira ili kupunguza kasi ya wapinzani wao, ambao walikuwa moto kusaka bao.

Dakika ya 60-80 ya mchezo, mambo yalibadilika na timu zote zikishambuliana kwa zamu na dakika ya 82 Shaw akitumia juhudi binafsi aliiweka mbele zaidi United kwa kupachika bao la pili na kumpa Mourinho uhakika wa pointi tatu muhimu.
 
Back
Top Bottom