Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aguero anakuwa mchezaji wa pili katika Ligi Kuu England kufunga hat trick ya tisa akimkaribia shujaa wa New Castle United, Alan Shearer aliyefunga hat trick 11, kwa muda wote wa uchezaji wake.

Mara baada ya kufunga bao la tano ambalo lilikuwa la tatu kwa Sergio Aguero, mfungaji bora wa muda wote wa City, alipumzishwa zikiwa zimesalia dakika tisa.
 
Ushindi huo umeirudisha City kileleni mwa Ligi Kuu, ikifikisha pointi sita na mabao manane ya kufunga na bao moja la kufungwa, ikiishusha Chelsea ambayo pia ina pointi sita lakini ikizidiwa mabao ya kufunga.

Katika mchezo mwingine wa Ligi hiyo, Burnley ikiwa nyumbani ilifungwa mabao 3-1 na Watford. Wakati mchezo utakaochezwa baadaye usiku wa leo utawakutanisha Brighton itakayoikaribisha Manchester United.
 
Rais wa Chama cha Soka Ujerumani (DFB), Reinhard Grindel, amemjibu Toni Kroos kwa kusema watamlinda Mesut Ozil dhidi ya ubaguzi.

Grindel alisema kuwa ubaguzi kwenye soka haukubaliki kwa namna yoyote ile, hivyo tofauti na anavyodhani Kroos, DFB itampigania na kumlinda kila mmoja anayebaguliwa.

Mashambulizi ya kibaguzi na shutuma kwamba alicheza chini ya kiwango katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia, zimemfanya Ozil kujitoa kuitumikia timu ya Taifa ya Ujerumani.
 
Nahodha wa Barcelona, Lionel Messi, jana aliifungia timu yake bao la 6,000 tangu ianze kushiriki Ligi Kuu ya Hispania, ilipoifunga Alaves mabao 3-0.

Bao la kwanza kati ya mawili aliyoyafunga kwenye mchezo huo ndilo lilifikisha idadi ya mabao 6000 kwa Barcelona tangu ianze kushiriki Ligi hiyo mwaka 1929 ikicheza michezo 2801.

Messi alifunga bao hilo dakika ya 64 kwa mpira wa adhabu uliopita juu ya ukuta wa Alaves, kabla ya mtokea benchi Philippe Coutinho kuongeza la pili dakika ya 83.
 
Nahodha wa Barcelona, Lionel Messi, jana aliifungia timu yake bao la 6,000 tangu ianze kushiriki Ligi Kuu ya Hispania, ilipoifunga Alaves mabao 3-0.

Bao la kwanza kati ya mawili aliyoyafunga kwenye mchezo huo ndilo lilifikisha idadi ya mabao 6000 kwa Barcelona tangu ianze kushiriki Ligi hiyo mwaka 1929 ikicheza michezo 2801.

Messi alifunga bao hilo dakika ya 64 kwa mpira wa adhabu uliopita juu ya ukuta wa Alaves, kabla ya mtokea benchi Philippe Coutinho kuongeza la pili dakika ya 83.
 
Wakati wengi wakiamini mchezo utamalizika kwa Barca kushinda mabao 2-0, Messi akafunga bao la tatu akionyesha uwezo mkubwa kwani alituliza kifuasi mpira aliopewa na Luis Suarez, akaumiliki na kuwapiga chenga mabeki wawili, akampiga chenga kipa na kuujaza mpira wavuni.

Mesi amezidi kujiwekea rekodi katika Ligi Kuu Hispania na kwa klabu yake kwani ndiye mchezaji aliyeifungia Barca mabao mengi zaidi, pia Februari 1, 2009 aliifungia bao la 5,000 walipocheza na Racing Santander.
 
Katika historia ya Ligi Kuu Hispania ni Real Madrid pekee ambayo imefunga mabao zaidi ya 6,000, ikiwa imefunga mabao 6,041 katika mechi 2,800.

Aidha mabao hayo yamemuwezesha Messi kufikisha mabao 385 katika La Liga yote akiwa ameifungia Barcelona.

Kati ya mabao hayo 6,000 ya Barca, walioandika rekodi kwa ufungaji ni, Manuel Parera aliyefunga bao la kwanza la timu hiyo katika Ligi mwaka 1929, Marco Aurelio akaifungia bao la 1,000 mwaka 1950 Pedro Zaballa akafunga bao la 2,000, mwaka 1964, bao la 3,000 likafungwa na Quini mwaka 1982, bao la 4,000 likafungwa na Guillermo Amor mwaka 1996 bao la 5,000, Lionel Messi mwaka 2009 bao la 6,000, Lionel Messi, Agosti 18, 2018.
 
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameirushia dongo timu hasimu ya Manchester City akisema licha ya kuwa na fedha zinazoweza kuipa wachezaji bora lakini haziwezi kununua ubora.

Licha ya kutokuwa na kikosi bora kama kile cha City, United iliichapa timu hiyo na kuichelewesha kutangaza ubingwa msimu uliopita, jambo linalompa Mourinho kiburi.

“Hamna ubishi kuwa Man City ni klabu tajiri England, lakini haina uwezo wa kununua ubora kwa utajiri huo,” alisema Mourinho.

Kocha huyo aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa kuhusu matumizi ya Pauni 10 milioni zilizotumiwa na klabu hiyo kuandika kumbukumbu za historia ya klabu hiyo kwenye maandishi na katika video, iliyozinduliwa wiki iliyopita.

Msimu uliopita City inayonolewa na Pep Guardiola, kutokana na ubora wa kikosi chake iliweka rekodi ya kutwaa ubingwa ikiwa imejikusanyia pointi 100.

Hata hivyo Mourinho alikumbushia kichapo walichoipa City Aprili 7 mwaka huu katika mechi ya Ligi Kuu kwenye dimba la Etihad, ambapo hadi mapumziko City ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 lakini United ilisawazisha na kushinda kwa mabao 3-2.

Mourinho alisema kuwa hajapata kuona klabu inayoweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuandika kitabu au kutengeneza filamu ya kumbu kumbu.

City iliyoanza Ligi ya msimu huu kwa kuichapa Arsenal mabao 2-0, leo itashuka kwenye dimba la Etihad kuikaribisha timu ngeni katika Ligi hiyo ya Huddersfield.
 
Mchezaji nyota wa zamani wa tenisi kutoka Marekani, Pete Sampras ameliweka sokoni jumba lake la kifahari lililopo Los Angeles.

Hata hivyo katika siku ya kwanza ya mnada Jumba hilo lililojengwa mwaka 2009, halikupata mnunuzi.

Mauzo ya jumla ya jumba hilo la Sampras ni Dola 8.9 milioni na kiasi hicho kwa mijengo iliyopo Los Angeles sio kitu.

Madalali wamelisifia jumba hilo wakisema lina vyumba viwili vya kupumzikia vyumba vine vya kulala, bafu sita, moja likiwa la sinki kubwa ambalo watu wawili wanaweza kuenea kwa wakati mmoja.
 
Pia walichimba bwawa la kuogolea, gereji ndogo pamoja, uwanja wa kuchezea tenisi na sehemu kubwa ya kupumzikia.

Hata hivyo haijaelezwa kuwa Sampras, bingwa wa mataji 14 ya Grand Slam na mkewe Bridgette Wilson-Sampras, anauza jumba hilo kutokana na kufilisika au la.

Wenza hao walinunua nyumba na eneo la ziada la uwanja kwa Dola 5.9 milioni mwaka 2009 kisha kujenga jumba hilo la kifahari Los Angeles Times.
 
Wachezaji nyota namba moja wa zamani wa tenisi duniani, Novak Djokovic na Roger Federer, leo wataonyeshana kazi kwenye fainali ya Cincinnati Masters.

Wachezaji hao waliowahi kushika namba moja kila mmoja kwa wakati tofauti, walitoana jasho katika nusu fainali ya mashindano hayo mwaka 2015, ambapo mashabiki walipata burudani ya uhakika kwani walitumia zaidi ya saa mbili kumka mshindi.
 
Novak Djokovic atakuwa akipigania kuandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda michezo yote tisa ya Masters 1,000, iwapo atatwaa taji hilo la Cincinnati Masters.

Nyota huyo kutoka Serbia, ambaye mara tano aliwahi kushika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo alimshinda Marin Cilic wa Croatia katika nusu fainali kwa 6-4 3-6 6-3.

Naye Federer, aliingia kwenye fainali baada ya mpinzani wake David Goffin wa Ubelgiji kuumia bega na kuamua kujitoa mashindanoni, hata hivyo wakati akijitoa walikua sare wakifungana seti 1-1.
 
Klabu ya Real Madrid, inadaiwa kumtengea mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani, Euro 70 milioni.

Habari zinasema kuwa oda iliyotolewa na nahodha wa Barcelona, Lionel Messi kwa klabu yake ndiyo iliyowazindua Real Madrid na kumtengea mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay kiasi hicho cha fedha.

Imeelezwa kuwa Real ilisikia Messi akiishauri Barca imng’oe Cavani PSG baada ya kusikia tetesi kuwa mpiga mabao huyo hana raha ya kuendelea kuwepo jijini Paris.
 
Baada ya kunasa tetesi hizo Real wakaamua kuifanyia kazi kutokana na kuogopeshwa na ubutu wa safu yao ya ushambuliaji baada ya kuondokewa na Cristiano Ronaldo.

Habari ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa PSG wako tayari kumuachia mshambuliaji huyo kwenda jklabu yoyote itakayotoa Euro 120 milioni.
 
Mbinu za Kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri za kushambulia muda wote zinaonekana kuzaa matunda baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Arsenal.

Chelsea ambayo msimu uliopita ilimaliza Ligi katika nafasi ya tano inaelekea msimu huu itarejea katika nne bora za Ligi Kuu England, nafasi ambazo zinatoa timu za kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sarri licha ya kuwa yupo katika msimu wake wa kwanza Stamford Bridge baada ya kumrithi Antonio Conte, ameanza vema alishinda mchezo wa kwanza ugenini kwa mabao 3-0 dhidi ya Huddersfield Town.

Ushindi dhidid ya Arsenal umeifanya Chelsea kukaa kileleni mwa Ligi kwa takribani saa 24, wakati Unai Emery aliyechukua nafasi ya Arsene Wenger, kuinoa Arsenal ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya sita.
 
Mbali ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo uliochezwa Stamford Bridge, Chelsea ilicheza soka la kuvutia liliwakuna mashabiki wa klabu hiyo.

Mashambulizi mfululizo katika kipindi cha pili yaliwalazimisha Arsenal kuachana na mfumo wao wa soka la gonga badala yake wakarudi nyuma kujilinda muda wote.

Kipigo hicho kwa Arsenal ni cha pili mfululizo baada ya kile cha mabao 2-0 walichokipata kutoka kwa Manchester City, wikiendi iliyopita ikiwa mara ya kwanza kupoteza mechi mbili mfululizo za kwanza tangu kuanzishwa kwa Ligi hiyo msimu wa 1992-93.
 
Back
Top Bottom