Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1cd7a3eb-c3df-4de3-929c-10621ad4ba17.jpg
 
*BREAKING NEWS: CHUO KIKUU MUHIMBILI KIMETANGAZA NAFASI KIBAO ZA AJIRA KWA WATANZANIA*


[emoji860][emoji860] *MUHIMBILI YAMWAGA NAFASI MPYA ZA AJIRA -MAOMBI YOTE YANATUMWA ONLINE*

Elimu: Kuanzia wahitimu wa kidato cha nne / Certificates /Diploma/Degree++

*Wanahitajika nafasi hizi*

[emoji828] Care takers(Social Workers)
[emoji828] Madereva wanahitajika
[emoji828] Secretaries wanahitajika
[emoji828] Wardens wanahitajika
[emoji828] Accounts Assistants
[emoji828] Library Officers wanahitajika
[emoji828] Artisians wanahitajika
[emoji828] Laboratory Technicians
[emoji828] ICT officers
[emoji828] Procurement& Supplies
[emoji828] Records Management Assistants
[emoji828] Nutritionists
[emoji828] Technicians wanahitajika
[emoji828] Nursing Officers wanahitajika
[emoji828] Assistant Nursing Officers
[emoji828] Health Attendants wanahitajika
[emoji828] Medical Doctors
[emoji828] Radiographers
[emoji828] Medical Record Assistants
[emoji828] Pharmacists
[emoji828] Administrative Officers
[emoji828] Medical Specialists
[emoji828] Lectures
[emoji828] Assistant Lectures wanHitajika
[emoji828] Tutorial Assistants
[emoji828] Reseach Fellows
[emoji828] Librarians

*Deadline: August 30,2018*

*Bonyeza Link Kufahamu Jinsi ya kutuma maombi Online-Link*
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Employment Opportunities at Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS),August 2018


*NAFASI NYINGINE MPYA ZA AJIRA BONYEZA HAPA*
[emoji117]Home

*SAIDIA KUSHEA*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tamaa ya ngono imewaponza wachezaji wanne wa timu ya Taifa ya Japan ya mchezo wa kikapu waliokwenda kushiriki mashindano ya ubingwa wa Mataifa ya Bara la Asia yanayofanyika Jakarta na Palembang nchini Indonesia.

Mkuu wa msafara wa timu hiyo Yasuhiro Yamashita, aliomba radhi kutokana na kitendo kilichofanywa na wachezaji hao akisema kimeidhalilisha Japan mbele ya jumuiya ya kimataifa.

“Tunaomba radhi kwa kilichofanywa na wachezaji hawa wameidhalilisha nchi na ili kuonyesha tumechukizwa na kitendo chao tumewaondoa kwenye timu ya Taifa na kuwarudisha nyumbani,” alisema Yamashita.
 
Aliwataja wachezaji hao waliowanunua makahaba ili kulala nao kuwa ni, Takuya Hashimoto, Keita Imamura, Yuya Nagayoshi na Takuma Sato.

Alisema kuwa wachezaji hao walikwenda kula chakula cha usiku na baada ya chakula wote wakawanunua makahaba wa kwenda kulala nao katika hoteli ambayo msafara mzima wa Japan umefikia.

Hata hivyo waliporejea hotelini na makahaba hao uongozi wa hoteli uliwazuia kuingia nao na baada ya mabishano kuzidi ikabidi wakuu wa msafara wa Japan wafahamishwe juu ya tukio hilo la wachezaji hao.
 
Japan ilipangwa kuanza kinyang’anyiro cha mashindano hayo upande wa kikapu kwa kucheza na Qatar kesho Alhamisi.

Wachezaji hao wameenguliwa kwenye timu na kurudishwa nyumbani kutokana na kuwanunua makahaba baada ya chakula cha usiku.

Indonesia ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya waislamu duniani, ambako hoteli nyingi zinafuata sheria za kiislamu ‘Sharia’ za kuzuia mwanamume na mwanamke asiye mke wa ndoa kuchanganyika kwa namna yoyote ile.
 
Mashindano hayo yaliyozinduliwa Jumamosi iliyopita yanatarajiwa kumalizika Septemba 2 mwaka huu mjini Jakarta.

Waandaaji wamesema kuwa jumla ya wanamichezo wapatao 18,000, kutoka mataifa mbali mbali ya Asia, wamekusanyika katika miji ya Jakarta na mji maalumu kwa mashindano hayo Palembang, ikishirikisha michezo zaidi ya 40.
 
MANCHESTER City wameanza utetezi wa ubingwa wao Ligi Kuu ya England (EPL), wakijua wazi wana mtihani mgumu, hasa kutoka kwa klabu nyingine kubwa tano hapa nchini.

Wapo chini ya Pep Guardiola na kwa historia ya hapa imekuwa ngumu kabisa kwa timu kutetea taji.

Karibuni kabisa ni jinsi Chelsea walivyotoka kwenye ubingwa hadi kutupwa nje ya nne bora na hivyo kukosa fursa ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) msimu huu.
 
Hata hivyo, kabla yao walikuwa ni Leicester City waliochukua ubingwa kwa kuwashangaza wengi, wakiwavuruga vigogo lakini ilipofika Januari ya msimu uliofuata walikuwa wakielekezwa kushuka daraja, ikabidi kocha aliyewapa kombe, Claudio Ranieri ‘Tinkerman’ afukuzwe kazi.

City walikuwa na msimu mzuri sana uliopita, wakiweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi na kupoteza mechi moja tu na walikuwa wakiitafuta rekodi ya Arsenal ‘The Invicible’ enzi hizo na hawakupoteza mechi hata moja msimu mzima.
 
Hata hivyo, pamoja na ufanisi wa wachezaji wake, kuna hisia safari ya City inaweza kuwa ngumu na huenda wakacharazwa na baadhi ya timu, baada ya kufikisha alama 100 msimu uliopita.

Je, itachukua muda gani kuaminisha watu hizi ni zama kama zile za Guardiola kule Bayern Munich au sehemu kubwa ya muda wake Barcelona? Je, atajulikana kwa mechi kadhaa za mtoano kwenye UCL?

Ushindi wa City dhidi ya Arsenal kwenye mechi yao ya kwanza EPL iliyotanguliwa na ushindi wa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea ni dhihirisho la awali tu la nguvu yao dhidi ya wale sita bora wa EPL, lakini akiwashinda makocha wapya kabisa England – Mhispania na Mtaliano Unai Emery na Maurizio Sarri mtawalia. City walishinda kilaini na hawakujaribiwa.
 
Timu mbili hizo zimejielekeza kucheza mfumo wa kushinikiza mipira mbele na laiti wangefanikiwa si ajabu wangefanya kile Liverpool walichowatenda City UCL kwa kuwachapa mabao ya kutosha kwenye mechi mbili humo na kuwatupa nje.

Tazama wachezaji waandamizi ambao hawakuwapo kwenye kikosi cha City ni pamoja na nahodha Vincent Kompany, Nicolás Otamendi, Phil Foden, Kevin De Bruyne, Leroy Sané na Gabriel Jesus waliokuwa pale benchi.
 
David Silva na Fabian Delph walikuwa nyumbani Manchester. Yeyote kati yao angekuwa uwanjani nguvu ingeongezeka sana.

Kama wapinzani wao wanavyopenda kusema, City wametumia kiasi kikubwa cha fedha, lakini walau kwa nyakati za karibuni, wamekitumia vyema na hakuna upotevu, maana Guardiola husajili wachezaji kuendana na mpango wake wa jinsi ya kuwatumia na si vinginevyo.

Hata hivyo, katika soka lolote laweza kutokea; nani angejua Leicester wangechukua ubingwa ule, au Chelsea wakawapiga Bayern Munich kule kwao Allianz Arena na kutwaa ubingwa wa Ulaya? Soka ni kwamba wakati mwingine ule uthabiti wa timu unaweza katika shinikizo kuwa udhaifu. Kuna matumaini gani kwa timu nyingine EPL basi? Wapo wanaoona kama City watakuwa kwenye mserereko wa ushindi.
 
Kwenye msimu wake wa kwanza, Guardiola aliwaongoza City kushinda mechi 10 mfululizo, ikachukuliwa City walikuwa wakiuendea ubingwa, lakini wakaja kuzuiwa kwa mechi sita zilizofuata wakishindwa kushinda, wakianza kwa sare.

Morali na hali ya wachezaji katika timu huweza kubadilika ghafla na matokeo vivyo hivyo na hii yawezekana sana kwenye klabu kama Man City yenye mfumo wa kifalme.

City wamekuwa na mabeki wanaopanda, kama Benjamin Mendy na Kyle Walker huku mawinga, Raheem Sterling na Riyad Mahrez wakikata na kuingia ndani kutoka wingi za kushoto na kulia mtawalia na wakapata mabao mawili dhidi ya Arsenal kupitia kwa Bernado Silva na Sterling ambaye ndani ya jezi ya Timu ya Taifa ya England – Three Lions, amekuwa akipata kigugumizi sana mbele ya lango.
 
Hata hivyo, hiyo haimaanishi wapo salama, maana wanafunguka kupita kiasi wanapokwenda kushambulia na laiti timu pinzani wafanikishe shambulizi la kushtukiza, hakika City wataumia.

Wakiwa na timu nzuri iliyojipanga na inayoona fursa, wanaweza kufungwa kirahisi kama walivyotendwa na Liverpool wa Jurgen Klopp.
 
Mmiliki wa klabu ya Leeds United, Andrea Radrizzani, amesema alitaka kumuajiri mmoja kati ya makocha wakubwa kuinoa timu hiyo ya Ligi Daraja la kwanza, lakini wakamtolea nje.

Radrizzani alisema kuwa mkakati wake ni kuona timu hiyo inarejea Ligi Kuu England na miongoni mwa mambo aliyoyafikiria ni kuajiri mmoja kati ya makocha wazoefu, Antonio Conte, Claudio Ranieri na Roberto Martinez.

Hata hivyo, makocha hao kila mmoja kwa sababu zake alimtolea nje ndiyo maana akaamua kumuajiri bakia na Marcelo Bielsa.
 
Radrizzani aliyeinunua Leeds Mei 2017, alisema alimpigia simu Conte na kumpa ofa ya Euro 20 milioni, kabla ya kutete na Claudio Ranieri na baadaye akaongea na Roberto Martinez.

Alisema pengine kutokana na kutarajia ofa kutoka moja ya klabu kubwa wote walimtolea nje ndipo akajadiliana na Mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo Victor Orta aliyesisitiza kuwa Bielsa atawafaa.

Alibainisha kuwa Kocha huyo aliridhia kitita cha Pauni 3 milioni pekee kwake pamoja na wasaidizi wake, kwa mkataba wa mwaka mmoja.
 
Back
Top Bottom