Kuweza kumbadili tabia mwenza wako Mojawapoya jambo ambalo hufanywa na wengi walio katika mahusiano ni kuwa na 'tamaa' yakutaka kumbadili tabia fulani mwenza wake. Hata hivyo 'tamaa' hii ni sehemu yayale tunayoyaita matarajio yasiyo halisi, kwani tabia ya mtu hujengwa na mambomengi sana, ikijumuisha aina ya makuzi, aina ya mfumo wa imani mtu anaouamini,aina ya marafiki alio nao, uwezo wake wa kujiamini katika kubadili tabia kwaniwengine wameshakata tamaa kuwa hawawezi kukata tamaa, na zaidi sana, mabadilikoya tabia huhitaji mfumo endelevu na wenye kusoma vema asili ya tabia ili kuwezakuirekebisha. Hatahivyo wengi wetu kwenye mahusiano, hutegemea 'mapenzi'au vitisho tuu kama
vile'nitakuacha mie ', kama sababu yakumfanya mtu abadilike kitabia.Udhaifu wetu katika kutambua asili
ya tabia yamtu husika na mbinu za kisayansi za kubadili tabia hufanya zoezi lakubadilishana tabia kuwa gumu na pengine lisilowezakana