Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry amekubali kuinoa klabu ya Bordeaux ya Ufaransa.

Klabu hiyo imeshamtimua kazi aliyekuwa kocha wake Gus Poyet, baada ya kukwaruzana na uongozi na alitishia kuondoka akipinga uongozi kumuuza mshambuliaji mahiri Gaetan Laborde kwenda Montpellier bila kusajili mbadala wake.

Ili kuficha ukweli uongozi wa klabu ukaamua kumfuta kazi kabla hajaanika mambo na sasa wanamshawishi Henry Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ubelgiji atwae mikoba hiyo.
 
Mshambuliaji huyo anayeshikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa, aliyewahi kuichezea pia Barcelona kabla ya kumalizia soka lake Marekani na kugeukia ukocha anasubiriwa kutoa mapendekezo kadhaa ikiwemo watu anaotaka wawe wasaidizi wake.

Aidha imeelezwa kuwa bodi ya ukurugenzi inapanga kumtwaa Arsene Wenger na kumpa jukumu la kuwa Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo.

Iwapo Henry mwenye miaka 41, atafanya kazi Bordeaux ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Arsenal pamoja na kwenye kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Dunia mwaka 1998 Patrick Vieira anayeinoa Nice.
 
443c5e8e78f24bb8617baf23c8a13cd8.jpg
 
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anazidi kuvurugwa baada ya aliyekuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kutajwa kuwa atamrithi Old Trafford.

Siku chache zilizopita, kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane alipohojiwa alisema kuwa anataka kazi Old Trafford na kuzidisha presha kwa kocha huyo.

Mourinho amekuwa na wakati mgumu kutokana na kuanza vibaya, mechi ya pili tu kwa timu yake kufungwa mabao 3-1 na Brington.

Kocha huyo anaonekana kuwa tatizo licha ya kuwa alikataliwa kusajili mabeki wa kati aliokuwa akiwalilia dirisha lililopita. Habari kutoka ndani ya viunga vya Old Trafford zinasema kuwa Makamu Mwenyekiti, Ed Woodward atamaliza tatizo na ni kama kumpa rungu Ed Woodward na kulimaliza kibabe suala la Mourinho.
 
HABARI ndiyo hiyo. Bayern Munich imedhamiria kuvunja rekodi ya dunia kwenye uhamisho wa wachezaji kwa kumnasa supastaa wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann. Ripoti kutoka Ujerumani zinadai wababe hao wa Bundesliga wamemweka Griezmann kwenye chaguo lao la kwanza kabisa la wachezaji inaowataka watue kwenye kikosi chao mwaka huu.

Lakini Mwenyekiti wa Bayern Munich, Uli Hoeness amesema wamepanga kufanya matumizi makubwa kwenye kusajili wachezaji kwa mwaka 2019. “Mwakani tutafanya usajili mkubwa, kwa sasa tunahitaji pesa zetu,” alisema Hoeness.
 
Bayern ipo tayari kutoa mkwanja wa Euro 200 milioni kumnasa Griezmann, pesa ambayo inaamini itaweza kumng’oa Mfaransa huyo kutoka Atletico Madrid.

Bayern inafanya maandalizi ya kutafuta wachezaji wa kuchukua mikoba ya maveterani, Arjen Robben na Franck Ribery.

Kama Griezmann atagoma, basi basi Bayern itahamishia nguvu kwa Paulo Dybala.
 
NI hivi, Shirikisho la soka la Ulaya (Uefa) limepanga kutambulisha matumizi ya video kufanya uamuzi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia hatua ya robo fainali. Uefa imepanga kuanza kutumia teknolojia hiyo ya video kumsaidia mwamuzi, VAR baada ya kuona mafanikio kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018, Russia.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Uefa teknolojia hiyo itaanza kutumika kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya klabu za Ulaya. Uefa pia inafikiria kuanza kutumia VAR kwenye michuano ya Euro 2020. Droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zitafanyika Agosti 30 mjini Monaco, Ufaransa.
 
SUPASTAA Cristiano Ronaldo ameamua kujivisha mabomu kuwa amehamia Juventus kwa ajili ya kazi moja tu, kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Staa huyo wa Ureno alihama Real Madrid kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi huko Ulaya na kwenda kujiunga na wababe hao wa Italia, huku mwenyewe akisema kuwapa ubingwa wa Ulaya Juventus ndicho kitu kilichomsukuma kujiunga na timu hiyo.

Ronaldo alianza msimu wake wa kwanza kwenye Serie A kwa ushindi baada ya Juventus kuichapa Chievo Verona, lakini staa huyo wa zamani wa Manchester United hakufunga wala kutoa asisti katika mechi hiyo.

“Nataka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya nikiwa na Juventus, nalifanyia kazi hilo na wachezaji wenzangu, lakini si kwa kuwa na pupa, tunakwenda hatua kwa hatua,” alisema.
 
Back
Top Bottom