SUPASTAA Cristiano Ronaldo ameamua kujivisha mabomu kuwa amehamia Juventus kwa ajili ya kazi moja tu, kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Staa huyo wa Ureno alihama Real Madrid kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi huko Ulaya na kwenda kujiunga na wababe hao wa Italia, huku mwenyewe akisema kuwapa ubingwa wa Ulaya Juventus ndicho kitu kilichomsukuma kujiunga na timu hiyo.
Ronaldo alianza msimu wake wa kwanza kwenye Serie A kwa ushindi baada ya Juventus kuichapa Chievo Verona, lakini staa huyo wa zamani wa Manchester United hakufunga wala kutoa asisti katika mechi hiyo.
“Nataka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya nikiwa na Juventus, nalifanyia kazi hilo na wachezaji wenzangu, lakini si kwa kuwa na pupa, tunakwenda hatua kwa hatua,” alisema.