capitalpool
JF-Expert Member
- Sep 18, 2017
- 22,369
- 121,270
Yes kwa kawaida huwa sipendi aibu, kwa vyovyote vile nisengemwangusha mwl wangu huyu. Shukurani zangu nyingi kwake Pyaar sito kuangusha.Kumbe darasa lilishaanza? Sikujua bro. Nafuta kauli yangu hapo juu. Na kwa prof kama yule mwezi mmoja tu tayari unakuwa na native speaker competence kabisa...Hongera bro [emoji122][emoji122][emoji122]
Hakuna msg inajibiwa haraka kama 'Pesa nitume kwenye namba gani'? [emoji1]
Ok, hebu tuanze hivi, ni mara ngapi ushawahi kuingia katika basi ukakutana na mwanamke mrembo ukamtamani? Ama ni mara ngapi ukiwa ndani ya gari ushawahi kumwona mwanamke mrembo ameingia na kukaa mbele yako? Ni mara nyingi. Mambo kama haya hutokezea kila siku. Mwanzo kila siku unapoabiri basi huwa unakutana na wanawake tofauti tofauti na warembo. Na je, unajua mbinu ya kuwaaproach uanze mazungumzo? Somo letu litafafanua kwa upana.
Wanawake wakiwa ndani ya magari ya usafiri huwa rahisi kuwaaproach tofauti na sehemu nyingine unazozijua. Hii ni kwa sababu ya mambo haya:
1. Kinga zake ameziweka chini. Katika gari za usafiri mwanamke huwa hayuko katika hali ya kutangamana, so hatakuwa na mawazo katika akili yake kama vile anavyokuwa katika kilabu. Mfano hafikirii mbinu za kukabiliana na wanaume wanaoudhi ama kuwa na wasiwasi wa kwanini hakuna mtu mpaka sahizi amemuaproach. Nguvu zake zote katika gari la usafiri huwa zimetulia ukilinganisha na wakati ameenda kula bata na marafiki zake usiku. Katika hali hii huwa ni rahisi kumuaproach na anaweza kuungana na wewe kirahisi bila matatizo.
Asante mkuu...KIZARAMO---Kibogwa
2. Gemu huwa ya juu. Katika magari ya usafiri wanawake ni wengi mno. Kila siku ukisafiri utakutana na wanawake tofauti. Wale ambao utakutana nao leo, si wale ambao utakutana nao kesho. Hii inamaanisha kuwa kadri utakapokuwa ukisafiri ndipo utakapokuwa na nafasi nzuri ya kuchagua mwanamke unayetaka wewe.
Asante Consuela...
3. Una mstari ambao unafanya kazi kila wakati. Kuanza mazungumzo na mwanamke ni rahisi katika magari ya usafiri. Sentensi kama, "Unasafiri ukielekea wapi?" Tayari inaweza kuamsha mazungumzo yasiyokuwa na mwisho.
Ok. Hapo juu tumeonyesha sababu muhimu ambazo zinafanya kuapproach mwanamke katika gari la usafiri kuwa rahisi kuliko zote.
Kuna aina tatu za kumtambua mwanamke abiria. Nazo ni kama zifuatazo:
Hali #1 Mumesimama nje ya gari la usafiri unangojea kuingia ndani ukamwona mwanamke unayempenda. Katika hali hii mara nyingi hutokea katika basi. Abiria wote wako nje wanangojea kuabiri basi, halafu ghafla ukakutana na mwanamke unayevutiwa. Hatua ya kufanya hapa ni rahisi. Unachotakiwa kuanza ni kwenda hadi pale alipo, simama karibu yake halafu umwambie, "Waah, leo abiria ni wengi/wachache. Hivi unaelekea wapi?" Hapa atakujibu bila wasiwasi wowote sababu kinga zake zote ameziweka chini (sababu tumeeleza hapo juu).