Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati mashabiki wa Manchester United wakikasirishwa na kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Tottenham katika dimba la Old Trafford, inaonekana kipigo hicho si chochote si lolote kwake.

Unaambiwa Mourinho amechukulia poa sana na kuwapigia makofi mashabiki waliokuwepo uwanjani usiku wa jana.

Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa kikosi cha Mreno huyo, baada ya kupokea kipigo wiki iliyopita kutoka kwa vibonde, Brighton.
 
Baada ya mechi ya jana Mourinho aliwashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono, akawapigia makofi na kuwapungia kwa skafu ya Man United. Kisha alikutana na mtangazaji wa Sky Sport na kuzungumza maneno kadhaa. “Mashabiki wa Manchester United hawasomi magazeti na hawaangalii luninga,” alisema.

Kisha akaeleza “Ujumbe wangu (kwa wachezaji) ulikuwa kama wa mashabiki, ujumbe ambao mashabiki waliwapa wachezaji ulikuwa ujumbe wangu, ulikuwa ule ule.
 
Unapocheza kwa namna unavyocheza, unapotengeneza unachokitengeneza, tunapokosa nafasi tulizokosa, wakati wa mapumziko kila mtu alikuwa amevunjika moyo lakini kulikuwa na ushawishi kwamba tunakwenda kushinda mechi.”

Mourinho akiwapungiwa skafu mashabiki wa Manchester United baada ya mchezo wa jana.

“Hata tulipopata matokeo yasiyotarajiwa ya magoli 2, namna timu ilivyoendelea kucheza mpaka kufungwa goli la 3, ujumbe wangu kwa wachezaji ulikuwa chanya na nina furaha kweli, mnyenyekevu kwa namna mashabiki walivyowaonyesha hisia zao kwa vijana. Ninafikiri ilistahili lakini wakati mwingine wachezaji hawapati wanachostahili, kwa hiyo tunapaswa kuwa wanyenyekevu kwa namna mashabiki walivyotuchukulia.”
 
Mourinho alikumbusha namna walivyozomewa na mashabiki baada ya kutolewa katika hatua ya 16 katika ligi ya mabingwa na Sevilla na kusema kuwa walistahili. Kisha akasema “Leo wachezaji wametoka uwanjani wakiwa wamepoteza mchezo nyumbani na walipigiwa makofi kwa sababu walistahili, kwa hiyo tunaendelea kujaribu, kujaribu, kujaribu.”

“Mabao yalikuwa mangapi? (akionyesha vidole vitatu). Hiki ni nini? Ni mataji matatu ya ligi niliyoshinda, mataji mengi zaidi kuliko makocha wengine 19 ukiwaweka pamoja. Mimi matatu, wao mawili. Heshima, heshima, heshima,” alisema.
 
Manchester United ilipoteza mchezo wa jana usiku dhidi ya Tottenham kwa mabao 3-0, katika uwanja wake wa Old Trafford. Wakijitahidi kucheza mpira wa kujilinda na kushambulia, walijikuta wakiruhusu mabao mawili ndani ya dakika 3 za mwanzo wa kipindi cha pili kabla Mbrazili Lucas Moura hajarudi wavuni dakika ya 84.

Mabao ya Spurs yalifungwa na Harry Kane na Lucas Moura akifunga mabao mawili.
 
Hivi sasa kila mmoja anasema lake kuhusu Manchester United, baada ya kuwa na mwanzo mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 26 kutokana na kushinda mchezo mmoja na kupoteza miwili ya mwanzo wa msimu.

Hilo linasababisha jambo la kwanza kufikiriwa ni kumfukuza Kocha Jose Mourinho, anayeanza msimu wake wa tatu tangu atue kuinoa United.

Hata hivyo mlinzi na nahodha wa zamani wa United, Gary Neville, ameonya kuwa litakuwa kosa kubwa iwapo uongozi wa klabu hiyo utamtimua kazi Mourinho kama suluhisho.
 
Neville alisema licha ya Man United kuchezea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Tottenham Spurs hapo jana kwenye uwanja wao wa Old Trafford, hakuna sababu ya kupaniki wala kumtimua kazi Mourinho.

Badala yake ameshauri ushirikiano uongezeke wawaunge mkono wachezaji wao kwa kuwa kipindi hiki cha mpito ni cha muda mfupi na mambo yatakaa sawa.

“Ninawasihi uongozi usimfute kazi Mourinho, amejitahidi kuisuka timu ya ushindi lakini bado hajakamilisha kazi nadhani ni muhimu sana kumuacha aendelee na kazi yake, tumuamini na tumpe ushirikiano zaidi,” alisema Neville.
 
Alisema yeye ana imani kubwa kuwa kocha huyo akiendelea kupewa muda ataisuka timu ya ushindi, akaonya wasirudie makosa waliyoyafanya kwa makocha Louis van Gaal na David Moyes waliowatimua baada ya kukosa mataji kwa muda mfupi.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mlinzi wa zamani wa Liverpool na England, Jamier Carragher ambaye amesema licha ya kufungwa na Tottenham lakini United ilicheza soka la kuvutia ambalo linatoa matumaini kuwa iliangushwa na washambuliaji wake kushindwa kutekeleza mipango yao na sio tatizo la kocha.
 
Mcheza tenisi mahiri wa Uingereza, Andy Murray ameanza vema kinyang’anyiro cha mashindano ya US Open.

Murray aliyekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwaka na nusu anapambana kutwaa taji lake la kwanza la Grand Slam mwaka huu baada ya kushindwa kushiriki kwenye mashindano ya Wimbledon.

Katika mchezo wa jana usiku uliofanyika kwenye viwanja vipya vya Louis Armstrong Stadium vilivyo kwenye eneo la Flushing Meadows, Murray alimshinda kwa mbinde James Duckworth wa Australia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…