Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Emmanuel Amunike amewapiga chini wachezaji watano wa Simba waliogoma kuingia kambini timu ya taifa kwa muda kuanzia jana isipokuwa Aishi Manula pekee aliyeingia jana. . Kocha huyo ametangaza kuongeza wachezaji wachezaji wengine watano kutoka vilabu vya ligi kuu. . Wachezaji wa Simba waliondolewa kikosini ni: Erasto Nyoni Hassan Dilunga Shomari Kapombe Jonas Mkude Shiza Kichuya : Walioongezwa ni Salumu Kimenya Salum Kihimbwa Paal Ngalema David Mwantika Frank Domayo Kelvin Sabato
 
Mo Salah ameripotiwa kutaka kuwaambia bodi ya chama cha soka cha Egypt EFA kujiuzulu kama watashindwa kuzuia mashabiki wasiwe wanamsumbua anapokuja katika majukumu ya Timu ya Taifa. Nyota huyo wa Liverpool amedai kuwa kipindi anapoenda kwenye timu ya Taifa mashabiki wa Egypt wamekuwa wakigonga mlango wake Hotelini usiku wote wakitaka 'autographs' na picha. Mwanasheria wa Salah, Abbas Issa ametuma barua kadhaa kwa Rais wa chama hicho cha soka, Hany Abo Rida akishitaki vitendo hivyo anavyofanyiwa mchezaji huyo. Vitu alivyovitaka Issa Katika barua aliyoituma EFA Agost 23 mwaka huu. . ➡️EFA wanatakiwa wawazuie watu kuweka kambi nje ya chumba cha Hotel cha Salah, wasimgongee saa za usiku kutaka Autographs na Picha, wasimzonge zonge akiwa mazoezini . . ➡️ Salah muda wote awe na Bodyguard wawili . Na pia Bodyguard wawe nje ya chumba chake hotelini muda wote, na ulinzi wa kutosha katika Floor atakayokuwepo. . ➡️ Simu zote zinazopigwa kuelekea chumbani kwake zizuiliwe . ➡️Salah hatakuwepo kwenye Promotion zozote, Mahojiano, mikutano, matukio ya wadhamini, ziara rasmi kwa niaba ya EFA. . ➡️Katika majukumu hayo ya Taifa,Salah anatakiwa kuchukuliwa uwanja wa ndege na EFA na kumpeleka moja kwa moja Hotelini kwa hadhi ya kipekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…