WAVUVI WATUMIA KONDOMU KULINDA SIMU ZAO BAHARINI, Pwani, Kenya.
”Sisi hutumia mipira hii ya kondomu ili kulinda simu zetu kutoingia maji wakati tunapokuwa baharini tukiendelea na shughuli zetu za uvuvi”, alisema mmoja ya wavuvi hao.
Mvuvi huyo anasema kuwa wanapoingiza simu zao za mkononi katika mipira hiyo zinasalia kuwa salama na ni rahisi wao kuzungumza na wateja wao walio nchi kavu mbali na kuitisha msaada wakati wa hatari baharini.
Katika jamii za kihafidhina kama hii inayoishi pwani ya Kenya, mipira ya kondomu hushirikishwa na tendo la ngono.
Hivyo basi ununuzi ama hata ubebaji wake ni swala linalozungumzwa kwa siri kubwa kutokana na kazi yake.
Kwa wengi ni mwiko kuonekana na kinga hiyo , hatua inayoweza kuwashangaza wengi unapopatikana ukitembea na mipira ya kondomu ambayo hazijatumika mfukoni.
Kulingana na wavuvi hawa swala la wao kuelekea nyumbani wakiwa wamebeba paketi za mipira hiyo limekuwa la kawaida.
”Kwa sasa wake zetu wamezoea kwamba wakati mwingi sisi hutumia mipira hii kuzuia simu zetu za mkononi kuingia maji tunapokuwa baharini. Lakini kitambo ilikuwa vigumu kuelezea unapokamatwa na mipira hii ambayo mara nyingi husahaulika katika mifuko lakini tulikuwa tukiwaelezea kwa umakini hadi wanaelewa”. alisema mvuvi huyo.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]