Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

download%20(40).jpg


Copyright @ 2018 AlfaPii
 
Mo Salah atumika
kutishia wapinzani
LIVERPOOL, ENGLAND
KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amewachimba mkwara wapinzani wake kwenye Ligi Kuu England akiwaambia kwamba staa wake Mohamed Salah amekuwa mtamu zaidi msimu huu kuliko vile alivyokuwa msimu uliopita, kwa hiyo mjipange.
Staa huyo wa kimataifa wa Misri alifunga mabao 44 katika kwenye kikosi cha Liverpool kwa michuano yote aliyocheza msimu uliopita, huku mabao 32 alifunga katika mechi 38 za Ligi Kuu England.
Kabla ya mechi ya jana Jumamosi kati ya Liverpool na Leicester City, Mo Salah tayari alikuwa amefunga mabao mawili na kocha Klopp anasema kwamba mchezaji wake kwa sasa anajiamini zaidi na amepevuka kufanya kweli ndani ya uwanja.
"Mo ni mtu safi sana. Hafikirii mambo ya msimu uliopita, anafikiria mambo ya mwaka huu. Anachotaka ni kuweka rekodi mpya," alisema Klopp.
"Si mtoto tena, anatambua kwamba mambo hayawezi kuwa kama ulivyotarajia siku zote, hivyo kama ni hivyo, basi ni lazima utapambana kwa nguvu zote kuweka mambo sawa."
Liverpool walicheza mechi yao ya mapema kabisa kwenye ligi jana huko uwanjani King Power.
 
Back
Top Bottom