Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

download.jpg


Copyright @ 2018 AlfaPii
 
Wakati wa mgogoro wa Zanzibar kuingia katika OIC na utaratibu wa kuchagua Makamu wa Rais,
yawezekana kuwa Rais mwenyewe aLikuwa akipendelea msimamo wa "Wazanzibari". Na hasa kuhusu suaIa la OIC, maelezo yake kwa Wazee wa Dar es Salaam na baadaye alipowahutubia wananchi siku ya Mei Mosi, Mtwara, yalifanya watu wengi waamini hivyo. Na washauri wake wa karibu walitaka tuelewe hivyo: kwamba ugumu wa suala la OIC ulikuwa unaletwa na Rais mwenyewe, maana alikuwa akiliona suala hila kwa jicho la Uzanzibari, badala ya kuliona kama Rais wa Tanzania na mlinzi mkuu wa katiba yake.
julius nyerere
 
Hatuwezi kuwa wakweli tukisema kuwa Rais hana hatia, Rais wa Tanzania si sawa na Malkia wa
Uingereza. Huyo ni Mkuu wa Nchi kikatiba ambaye hana madaraka ya kuongoza nchi yake. Kwa
mujibu wa Katiba na mazoea ya nchi yao hana budi akubali ushauri wa Waziri Mkuu wake, Hata kama yeye mwenyewe binafsi hakubaliani na ushauri huo. Rais wa Tanzania sivyo alivyo. Yeye ni Mkuu wa nchi Mtendaji. Kikatiba halazimiki kukubali na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu ambalo hakubaliani nalo, hasa kama tofauti yenyewe ni kwa jambo la msingi, kama vile jambo la maadili na dhamiri, au sheria, au Katiba ya Nchi
julius nyerere
 
Kutoka kwa Dotto Bulendu

Hapa ndipo "strong media" na "active citizens" wanatakiwa.

Kwanza tuliambiwa,wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi watachangia kutatua kero za elimu Dar es Salaam,makontena ya vifaa vya ofisini na vitabu yatakuja kutoka ughaibuni.

Baadae tukaambiwa si hayo tu bali na mengine yatatoka China kwa ajili ya maziwa ya watoto waliotelekezwa na mengine yataleta vitabu kwa ajili ya maktaba.

Baada ya hapo tukaambiwa Makontena yamefika yapo 36 yanavifaa vya maofinini kwa ajili ya ofisi za walimu kwa Shule za Dar es Salaam.

Baadae tukaambiwa hayatoki mpala yalipiwe kodi kwani yamekuja kwa anuani ya mtu binafsi.

Baade tukaambiwa,kama TRA watataka yalipiwe kodi,wao na waziri wa fedha watashtakiwa kwa Rais.

Baadae tukaambiwa yanapigwa mnada ila yakapungua mpaka 20.

Baadae tukaambiwa atakaeyanunua atalaaniwa.

Baadae tukaambiwa,lazima yalipiwe kodi na aliyeyaleta na kama hatalipa yatapigwa mnada.

Baadae tukasikia waziri akisema,kama sheria ya kodi itapindishwa katika hili atakuwa tayari kumuomba Rais aachie ngazi.

Baadae tukamsikia Rais akisema,makontena hayo kwanza yana masofa na lazima yalipiwe kodi.

Baadae tukaambiwa mnada utapigwa leo jumamosi,

Baadae tunaambiwa mnunuzi kakosekana

Na sasa tunaambiwa kuwa kwanza hayo makontena hayana masofa kama tulivyoambiwa na vitu ni vichache sana eti vikipangwa vizuri yatabaki makontena yasiyozidi nane.

Haya mambo hayaaaaaa
Akili za kuambiwa changanya na za kwako.Ila kaeni mkijua Tanesco wameshindwa kesi ya Standard Chartered na wanatakiwa kulipa mabilioni ya shilingi.

Chaguzi ndogo nazo zinaendelea,na pia jueni kuna kundi kubwa la vijana lililomaliza vyuo vikuu,vyuo na kwenye taasisi za elimu ya juu wanasubiri ajira tangu mwaka 2015.

Wasalaaam.
Duh!
 
Katika maisha yako, kua mvumilivu kama *FUSO*,

Jipe moyo kama *BAJAJ*,

Usiwe na tamaa kama *DALADALA*,

Uwe jasiri kama *SCANIA*,

Uwe mstaarabu kama *COASTER*,
Na usijikweze Kama *NDEGE* Tena usiwaweke watu Roho juu Kama *MTUMBWI*
Maisha ni taratibu Kama *TREKTA*

hivyo usiwe na haraka kama *BODABODA*,

Waheshimu wenzako kama *BAISKELI*
, kuwa mpole kama mtembea kwa *MIGUU*.

Week.end njema.

Duuuu, mkuu unatisha[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom