Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

445730369_342607.jpg
 
Wakati tayari fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019 zikiwa zimepangwa kupigwa katika mji wa Madrid nchini Hispania, hizo zinaweza kuwa fainali za mwisho katika miaka ya hivi karibuni, kuchezwa ndani ya Ulaya.

Imefichuliwa kuwa upo mpango na mazungumzo yamefikia hatua ya juu, kuhakikisha mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya unachezwa Marekani kama ilivyokuwa kwa baadhi ya michezo wa Ligi Kuu Hispania โ€˜La Ligaโ€™.

Lengo la kuhamisha mechi hizo za fainli ni kuwahamisha wamarekani kupenda soka kwa upande mmoja na upande wa pili Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) likihitaji kujinufaisha kiuchumi kutokana na mapato ya viingilio na matangazo ya kibiashara.
 
Gazeti la London Evening Standard la Uingereza pamoja na kituo cha televisheni mjini Barcelona na Rร dio's 'El Mati ya Catalunya, nchini Hispania vimefichua juu ya mpango huo huku mtendaji mkuu wa Tv ya Mediapro iliyopo Barcelona, Jaume Roures, akisema anao ushahidi wa kutosha.

Roures alisema kuwa maafikiano ni kuwa mechi ya fainali ya mwaka 2020 au 2021 zipigwe mjini New York na zinazofuata zipigwe kwenye miji mingine ya Marekani.

โ€œKwa namna mazungumzo yalipofikia ni wazi kwamba fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2020 zitachezwa nje ya bara la Ulaya, itachezwa mjini New York,โ€ alisema.
 
Kocha wa England, Gareth Southgate ameweka bayana lengo lake ni kubadili namba ya beki wa Manchester City, Kyle Walker katika kikosi chake.

Walker alingโ€™ara katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Russia mwaka huu, licha ya kuchezwa katika nafasi isiyo yake ya mlinzi wa pembeni kushoto badala ya kulia alikozoea lakini alicheza kwa umahiri mkubwa.

Kocha wa England, Southgate amemwambia mlinzi huyo asiwe na wasiwasi wa kukosa namba kwani sasa anafikiria kumtumia kama mlinzi wa kati, kutokana na kujituma kwake pamoja na umakini alionao uwanjani.
 
Kutokana na tatizo lililojitokeza katika mechi za hivi karibuni nimepanga kuanza kumtumia Walker kama mlinzi wa kati badala ya kucheza pembeni, tuna tatizo katika eneo hilo,โ€ alisema Southgate.

Kocha huyo alifichua kuwa mbali ya mlinzi huyo pia atajaribu kuwachezesha katika nafasi hiyo, Joe Gomez, Kieran Trippier na chipukizi anayeichezea Liverpool mwenye miaka 19, Trent Alexander-Arnold.
 
Back
Top Bottom