Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanamuziki anayetamba na wimbo ‘Iokote’ Maua Sama na mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu, Soudy Brown wameendelea kusota rumande tangu walipokamatwa Septemba 16, 2018.

Wasanii hao walikamatwa sambamba na meneja wa Maua, Fadhili Kondo na wote wanashikiliwa kwa kosa la uharibifu wa mali ya umma baada ya kuonekana mtandaoni wakirusha hela na kuzikanyaga.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Septemba 19, 2018 msemaji wa nyumba ya vipaji (THT), Rehema Jones amesema mpaka sasa watatu hao bado wanashikiliwa na polisi.

Akielezea zaidi Rehema amesema walikamatwa Jumapili na taarifa za kukamatwa kwao zilifika THT siku ya Jumatatu.

Alipoulizwa kuhusu maendeleo yao na iwapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Rehema amesema, “utaratibu ndio unafanyika kuhusu suala la Mahakama na sisi tunasubiri kuona nini kitaendelea, kwa sasa hatuna zaidi cha kuzungumza.”

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu idadi ya wasanii ambao inasemekana wameendelea kukamatwa kufuatia sakata hilo, Rehema amesema; “THT ina taarifa za watu watatu tu, hao wengine hatuwezi kuwazungumzia.

Mwandishi wa MCL Digital ambaye yupo katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, anaripoti kuwa kitengo kinachoshughulika na makosa ya mtandao kimemweleza kuwa hakiwezi kutoa taarifa kwa kuwa wao si wasemaji.

“Nimeelezwa kuwa taarifa kuhusu watuhumiwa hao nitaipata kwa Kamanda wa Kanda kwa kuwa wao kazi yao ni kuwahoji watuhumiwa na kutafuta ushahidi kisha wanakabidhi kwake,” anasema Fortune.

Alipomtafuta Kamanda wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa alimweleza kuwa yupo katika ziara ya kikazi Kigamboni jijini Dar es Salaam na kumuomba amtafute jioni ampatie taarifa kamili.
 
Korea Kaskazini imekubali "kufunga kabisa" injini za kufanyia majaribio ya makombora pamoja na eneo la kurushia la Tongchang-ri, "huku wakishuhudia wataalamu kutoka kwa mataifa husika," imefahamika.
Hayo yameelezwa Jumatano na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in baada ya mkutano wa kilele na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un jijini Pyongyang.
Pia Moon alisema Kim atafanya ziara ya kihistoria katika Korea Kusini "siku chache zijazo".
Viongozi hao wametia saini azimio la pamoja mwishoni mwa majadiliano yao katika siku ya pili. Walikubaliana kuwa watafanya kazi kuifanya Rasi ya Korea kuondokana na tishio la nyuklia.
Moon ambaye alikwenda Kaskazini kwa ajili ya kupata mwelekeo mpya kukwamua mazungumzo yaliyokwama katika jitihada za kuondoa kabisa silaha za nyuklia, alisema ziara hiyo inaweza kufanyika mwaka huu labda tu yawepo "mabadiliko maalum".
Kuhusu suala lililompeleka la silaha, Moon alisema Kaskazini imekubali "kufunga kabisa" injini zake katika tukio ambalo watahudhuria wataalamu wa masuala ya silaha za nyuklia na makombora.
Korea Kaskazini imefanya majaribio na kurusha makombora kutoka eneo la Sohae, ambako licha ya programu yake ya makombora kupigwa marufuku na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, bado alitumia maeneo kadhaa mengine kurusha maroketi ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa Pyongyang.
 
Picha za setelaiti zilizopigwa Agosti zilionyesha wafanyakazi wakifungua injini za kufanyia majaribio ukiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyompa Rais Donald Trump wa Marekani.
Moon pia alisema Kaskazini inaweza kufunga kituo cha nyuklia cha Yongbyon ikiwa Marekani itachukua “hatua zinazolingana” ikiwa ni tahadhari muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…